Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • KAZI YA KUHUBIRI YAENEA KASKAZINI

      Mnamo Juni 1956, Ken na Rosina Frame, mapainia waliokuwa wametoka tu kuoana walikuwa Mashahidi wa kwanza kuhamia New Ireland, kisiwa kimoja kati ya Visiwa vya Bismarck vilivyoko kaskazini-mashariki mwa Papua New Guinea. Ken, aliyekuwa mhasibu, alifanya kazi katika kampuni kubwa huko Kavieng, mji mkuu wa kisiwa hicho. “Kabla ya kuondoka Sydney,” Ken anaeleza, “tulishauriwa kwamba tuwaache watu watuzoee kabla ya kuanza kuhubiri hadharani. Rosina alikuwa mshonaji stadi wa nguo na baada ya muda mfupi alikuwa na wateja wengi. Tuliwahubiria kwa njia isiyo rasmi, na baada ya muda kukawa na kikundi kidogo cha watu waliopendezwa ambao walikutana kwa siri nyumbani kwetu mara moja kwa juma.

      “Miezi 18 baadaye, mwangalizi wa mzunguko, John Cutforth, alitutembelea na kuuliza ikiwa angeonyesha sinema yenye kichwa The Happiness of the New World Society. Nilizungumza na mmiliki wa jumba la sinema, naye akakubali kuonyesha sinema yetu ya bila malipo. Lazima wafanyakazi wake waliwaambia watu wengine kuhusu sinema hiyo kwani tulipofika kwenye jumba hilo, lango lake lilikuwa limejaa watu, na tulihitaji msaada kutoka kwa polisi ili tufaulu kuingia ndani. Zaidi ya watu 230 walikuja kuitazama, bila kuhesabu watu waliochungulia kwenye madirisha yaliyokuwa wazi. Baada ya hapo tulihubiri waziwazi.”

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 99]

      Rosina na Ken Frame

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki