Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • KUHUBIRI KWENYE NYANDA ZA JUU

      Katika mwezi huohuo, Tom na Rowena Kitto walitoka Port Moresby na kufunga safari ngumu ya majuma kadhaa. Walikuwa wakielekea maeneo ambayo hayajahubiriwa kwenye nyanda za juu za New Guinea.

      Miaka 30 mapema, Waaustralia waliokuwa wakitafuta dhahabu waliingia kwenye nyanda hizo na kugundua karibu watu milioni moja ambao hawakuwa wamewahi kuwasiliana na sehemu nyingine za dunia. Wenyeji hao waliopigwa na butwaa walidhani wanaume hao wazungu walikuwa roho za mababu wao waliokuwa wamefufuka.

      Baada tu ya watu hao waliokuwa wakitafuta dhahabu, wamishonari wa dini zinazodai kuwa za Kikristo walifuata. “Wamishonari hao waliposikia kwamba tunaenda huko, waliwaamuru wanakijiji wasitusikilize,” anasema Rowena. “Lakini onyo lao lilitusaidia sana. Watu hao wa nyanda za juu—ambao kwa kawaida ni wadadisi—walikuwa wakitusubiri kwa hamu tufike.”

      Tom na Rowena walifungua duka dogo huko Wabag, kilomita 80 kaskazini-magharibi ya mji wa Mlima Hagen. “Makasisi waliwaagiza wafuasi wao wasinunue chochote kutoka kwetu, wasituuzie, au hata kuzungumza nasi na wakawashinikiza waombe tunyang’anywe ardhi yetu,” anasema Tom. “Hata hivyo, baada ya muda, wanakijiji hao waliona kwamba tulikuwa tofauti na wazungu wengine ambao waliwafahamu. Jambo lililoonekana wazi ni kwamba tuliwatendea kwa fadhili. Kwa kweli, mara nyingi matendo yetu ya fadhili yaliwafanya walie machozi na wakasema kwamba walitaka tuendelee kuishi huko!”

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • ◼ WAKATI Tom na Rowena Kitto walipofika Wabag, Mkoa wa Enga, wamishonari wenyeji walieneza habari za uwongo kuwahusu. Kwa mfano, wamishonari hao walidai kwamba Tom na Rowena waliifukua miili ya wafu na kuila. Uvumi huo uliniogopesha sana.

      Siku moja Tom alimwuliza baba yangu ikiwa alijua msichana fulani ambaye angeweza kumsaidia mke wake kufanya kazi za nyumbani. Baba alimweleza kwamba ningekuwa tayari kufanya hivyo. Niliogopa sana, lakini baba alinilazimisha nifanye kazi hiyo.

      Baadaye, Tom na Rowena waliniuliza, “Unafikiri ni nini huwapata watu wanapokufa?”

      “Watu wazuri huenda mbinguni,” nilijibu.

      “Je, ulisoma hivyo katika Biblia?” waliuliza.

      “Sijawahi kwenda shule, kwa hiyo sijui kusoma,” nikajibu.

      Walianza kunifundisha kusoma, na pole kwa pole nilianza kuelewa kweli za Biblia. Nilipoacha kuhudhuria Kanisa Katoliki, mmoja wa viongozi wa kanisa hilo aliniuliza: “Kwa nini uliacha kuja kanisani? Je, wazungu hao wawili wamekula moyo wako?”

      “Ndiyo,” nikajibu, “nimewapa moyo wangu wa mfano kwa sababu ninajua kwamba wananifundisha kweli.”

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 110]

      Tom na Rowena Kitto wakiwa mbele ya duka lao dogo na nyumba yao huko Wabag

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki