Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Raho na Konio Rakatani, Oda Sioni, Geua Nioki na mume wake, Heni Heni aliyekuwa amepata vichapo kutoka kwa wahubiri waliowasili katika mashua inayoitwa Lightbearer miaka 16 mapema, ni baadhi ya wale ambao walichukua msimamo imara kwa ajili ya kweli. Punde si punde, watu 30 hivi walikuwa wakihudhuria mikutano kwa ukawaida katika nyumba ya Heni Heni. “Wanaume waliketi upande mmoja na wanawake upande ule mwingine katika chumba hicho,” anakumbuka Oda Sioni, ambaye alikuwa kijana wakati huo. “Wanawake walivalia sketi za nyasi na hawakuwa na blauzi na waliwabeba watoto katika mifuko yenye kuvutia iliyofumwa kwa nyuzi na ilining’inizwa kwenye nguzo za chumba hicho. Baada ya kuwanyonyesha watoto, waliwatia ndani ya mifuko hiyo na kuibembeza polepole hadi watoto walipolala.”

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 78]

      Wahubiri wa kwanza wenyeji, kuanzia kushoto kuelekea kulia: Bobogi Naiori, Heni Heni Nioki, Raho Rakatani, na Oda Sioni

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki