-
Papua New Guinea2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
“Tulihubiri mahali popote tulipopata watu,” anakumbuka Elsie Thew, ambaye alitumika huko Papua New Guinea akiwa na Bill, mume wake, kuanzia mwaka wa 1958 hadi 1966. “Tulizungumza na watu vijijini, nyumbani, shambani, sokoni, na katika njia za vichakani. Tulizungumza na wavuvi katika fuo na kingo za mito. Mwanzoni tulipoanza kuhubiri katika eneo hilo, tulibeba ramani ya dunia yote ili tuweze kuwaonyesha watu waliokuwa sehemu za mbali sana mahali tulipotoka. Hilo lilikuwa muhimu kwa sababu tuliwasili kwa ndege, na kwa kuwa wanakijiji wengi hawakujua mengi kuhusu sehemu nyingine za dunia, walidhani tulianguka kutoka mbinguni! Kwa hiyo tuliwaonyesha kwamba tulitoka sehemu nyingine ya dunia ileile ambayo wao wanaishi.”
-
-
Papua New Guinea2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 127]
Elsie na Bill Thew
-