Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Chini ya hali hizo zenye mkazo, baadhi ya watu wanaopendezwa waliacha kujifunza. Hata hivyo, wachache walisimama imara. Mnamo 1954, ubatizo wa kwanza wa Mashahidi wa Yehova kufanywa nchini Papua New Guinea ulifanywa katika Mto Laloki huko Haima, na wanafunzi 13 wa Biblia wakabatizwa. Mmoja wao alikuwa Bobogi, ambaye alisema hivi: “Hata ikiwa watu wote wa Koiari wataacha kweli, mimi sitafanya hivyo, kwa sababu ninajua hii ndiyo kweli.” Kupatana na maneno yake, Bobogi alidumisha utimilifu wake, akitumika kwa uaminifu akiwa mzee katika Kutaniko la Haima hadi alipokufa katika mwaka wa 1974.

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ziara ya John ilifikia mwisho wakati wa kusanyiko la mzunguko la siku moja huko Haima. “Wanaotaka kubatizwa walipoombwa wasimame, . . . watu 70 walisimama!” anakumbuka Tom Kitto. “Mioyo yetu ilijawa na shangwe tulipoona ndugu 40 na dada 30 wakisimama msituni kwenye ukingo wa mto wakiwa tayari kuonyesha wakfu wao kwa Yehova.”

      Mwaka uliofuata, akina ndugu walipanga kuwa na kusanyiko la pili la mzunguko huko Haima. Bobogi, chifu wa kijiji, alipewa mgawo wa kutayarisha mahali pa kusanyiko na chakula kwa ajili ya wote waliotazamiwa kuhudhuria. Siku tatu kabla ya kusanyiko, John (Ted) Sewell, mwangalizi mpya wa mzunguko kutoka Australia, alikutana na Bobogi kuzungumzia matayarisho hayo.

      “Umejenga nini?” akauliza Ted moja kwa moja.

      “Hakuna,” Bobogi akamjibu.

      “Bobogi, leo ni Alhamisi (Siku ya 4) na kusanyiko ni Jumapili!” Ted akasema kwa mshangao.

      “Ni kweli, ndugu,” akajibu Bobogi. “Tutatayarisha kila kitu Jumamosi.”

      Ted alishangaa na kurudi Port Moresby akiwa na uhakika kwamba hakutakuwa na utaratibu wowote katika kusanyiko hilo.

      Jumapili hiyo alielekea Haima akiwa na wasiwasi kuona ni nini ambacho kingetukia. Kulikuwa na mabadiliko makubwa kama nini! Chini ya mti mkubwa kulikuwa na jukwaa la mbao mbele ya eneo kubwa lililokuwa limefyekwa. Mbali kidogo kulikuwa na maeneo ya kupikia, ambako nguruwe, wallaby, mbawala, hua, samaki, viazi vikuu, na viazi vitamu vilikuwa vikichomwa. Birika za chai zilikuwa zikichemka. Watu walichangamana kwa furaha katika eneo la kula lililotengenezwa kwa vifaa vilivyopatikana msituni. Bobogi alisimama katikati ya hekaheka hizo zote, bila wasiwasi wowote. Ted alistaajabu sana!

      “Bobogi, ulijifunzia wapi kufanya mambo haya yote?” akamwuliza.

      “Oh, niliona mambo yote haya katika sinema ile ambayo John Cutforth alituonyesha mwaka uliopita,” Bobogi akajibu.

      Zaidi ya watu 400 kutoka katika makabila manane walihudhuria kusanyiko hilo, na 73 wakabatizwa. Miaka iliyofuata, kusanyiko hilo likaja kuitwa kusanyiko la Bobogi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki