Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Lakini ni wapi ambapo wangetumika vizuri zaidi? Ofisi ya tawi ya Australia ilitoa jibu—Madang.

      Huko Madang, mji ulioko kaskazini-mashariki mwa pwani, “mashamba” yalikuwa tayari kuvunwa. (Yoh. 4:35) Kwa kweli, kikundi hicho kidogo cha wahubiri hakingeweza kushughulikia watu wote waliopendezwa. Painia Mkanada Matthew Pope na familia yake walipofika na kununua nyumba yenye vyumba kadhaa upande wa nyuma, njia ilifunguka ya kuwatuma mapainia wengi zaidi huko.

      Mapainia wanane waliwasili kutoka Rabaul na wakaishi katika sehemu mbalimbali za Wilaya ya Madang. Mmoja wao, Tamul Marung, alinunua baiskeli na kusafiri kwa kutumia mashua hadi Basken, kijiji cha nyumbani kwao, kilomita 48 kaskazini ya Madang. Baada ya kuhubiri huko Basken, alipanda baiskeli yake na kurudi Madang, akihubiri njiani. Kisha alirudi Basken, akaanzisha kutaniko, na kufanya upainia kwa miaka mingine 25. Katika kipindi hicho, alioa na akapata watoto. Baadaye, binti na mpwa wake wa kike walitumika Betheli.

      Wakati huo, huko Madang, John na Lena Davison walikutana na Kalip Kanai, mwalimu wa shule katika kijiji kidogo cha Talidig, kilichoko katikati ya Basken na Madang. Baada ya muda, John na Lena walikuwa wakisafiri hadi Talidig wakajifunze na Kalip na watu wake wa ukoo. Hilo lilimkasirisha mkaguzi wa shule aliyekuwa Mkatoliki, naye akawaamuru polisi wamfukuze Kalip na watu wake wa ukoo kutoka nyumbani kwao. Bila kuvunjika moyo, kikundi hicho kilihamia katika kijiji cha karibu cha Bagildig, na mwishowe kikawa kutaniko kubwa. Baadaye walijenga Jumba kubwa la Ufalme ambalo lilitumiwa kwa ajili ya makusanyiko. Sasa kuna makutaniko saba na vikundi viwili katika Wilaya ya Madang.

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 101]

      ‘Hatutaacha Kamwe’

      KALIP KANAI

      ALIZALIWA 1922

      ALIBATIZWA 1962

      MAELEZO MAFUPI KUMHUSU Alikuwa miongoni mwa ya watu wa kwanza kuikubali kweli katika eneo la Madang. Limesimuliwa na mwana wake, Ulpep Kalip.

      ◼ BABA yangu alikuwa mtu mnyenyekevu na alifikiria mambo kwa uzito. Alipokabili tatizo, angesikiliza kwa makini kisha achanganue jambo hilo kabla ya kutoa maoni yake.

      Nilipokuwa na umri wa miaka 15, nililazwa hospitalini huko Madang kwa sababu papa aliukata mguu wangu. Baba yangu alipokuwa akinitembelea, alikutana na John Davison. “Katika ulimwengu mpya,” John alisema, “Yehova anaweza kumpa mwana wako mguu mpya.” Baba yangu alipendezwa sana, hivyo akaanza kujifunza Biblia kwa bidii, na muda mfupi baadaye akawa na imani yenye nguvu.

      Kwa sababu baba yangu pamoja na watu wa familia yake walikuwa wamejiuzulu kutoka Kanisa Katoliki, polisi walichochewa watufukuze kutoka nyumbani mwetu. Nyumba zetu 12, zilizozungukwa na bustani zenye maua, zilikuwa bado hazijamaliza mwaka mmoja tangu zilipojengwa. Polisi walitupa mienge juu ya paa za nyasi, ambazo ziliteketea. Tulikimbia ili kuokoa mali zetu, lakini majivu yenye moto pamoja na moshi ulitushinda nguvu na kutufanya tutoke nje. Tulilia sana tulipoona nyumba zetu zikiteketea na kuwa majivu.

      Tukiwa na majonzi mengi tulitembea hadi Bagildig, kijiji jirani, ambako chifu wa kijiji hicho alikubali kwa fadhili tuhamie na kuishi kwenye kibanda kimoja. Tulipokuwa huko, baba yetu alituambia: ‘Yesu aliteswa. Kwa hiyo sisi pia tunatarajia kuteswa, lakini hatutaacha kamwe kushikilia imani yetu!’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki