Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • ◼ MNAMO 1980, painia mmoja alinipa trakti nikiwa Madang na nikaenda nayo hadi nyumbani katika Kisiwa cha Bagabag, umbali wa saa sita ukisafiri kwa kutumia mashua. Nilipendezwa sana na yale niliyosoma na nikaiandikia ofisi ya tawi barua ili nipate habari zaidi. Muda mfupi baadaye nilipokea barua kutoka kwa Badam Duvun, painia aliyeishi Madang, akinikaribisha kuhudhuria kusanyiko la wilaya. Nilimtembelea kwa majuma mawili na nikaanza kujifunza Biblia. Pia nilihudhuria mikutano yote katika Jumba la Ufalme la eneo hilo.

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Baba yangu alichukua chuma na kunifukuza kutoka nyumbani. Nilikimbilia Madang pamoja na shangazi yangu Lamit Mareg, ambaye pia alikuwa amekubali kujifunza Biblia. Muda mfupi baadaye, sote wawili tulibatizwa.

      Kisha, baba yangu akawa mgonjwa sana. Nilimkaribisha nyumbani kwangu Madang na kumtunza hadi alipokufa. Katika kipindi hicho, alikuwa na maoni tofauti kuelekea dini yangu. Kabla hajafa, alinisihi nirudi kwenye Kisiwa cha Bagabag na kuwahubiria wakaaji wa huko.

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Baadaye, nilirudi Madang ili nifanye upainia pamoja na Lamit. Mnamo 2009, watu sita kutoka Kisiwa cha Bagabag walisafiri hadi Madang ili kuhudhuria Ukumbusho wa kifo cha Kristo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki