Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Kwa mfano, karibu na mwaka wa 1970, ofisi ya tawi ilianza kupokea ripoti za utumishi wa shambani kutoka kwa mtu asiyejulikana, aliyekuwa katika kutaniko lisilojulikana, na katika kijiji kisichojulikana kwenye Mto Sepik ulio mbali sana. Ofisi ya tawi ilimwomba Mike Fisher, mwangalizi wa mzunguko, achunguze jambo hilo.

      “Ili kufika kwenye kijiji hicho, nilisafiri saa kumi kwa mtumbwi wenye injini kupitia mto mwembamba uliopita katikati ya msitu uliojaa mbu,” anaeleza Mike. “Mwishowe, nilifika jioni sana, na nikakutana na mtu huyo aliyekuwa ametengwa na ushirika miaka mingi mapema katika eneo lingine. Alirudi katika kijiji chake, akatubu dhambi zake, na kuanza kuwahubiria watu. Zaidi ya watu 30 katika kijiji hicho walijiita Mashahidi wa Yehova na wengine wao walistahili kubatizwa. Muda mfupi baadaye, mtu huyo aliyetubu alirudishwa, na kikundi hicho kikatambuliwa rasmi na ofisi ya tawi.”

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 115]

      Mike Fisher akiwa kwenye Mto Sepik

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki