Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Timotheo—Msaidizi Mpya wa Paulo
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
    • Paulo na Timotheo

      HADITHI YA 110

      Timotheo—Msaidizi Mpya wa Paulo

      KIJANA unayeona hapa pamoja na mtume Paulo ni Timotheo. Timotheo anakaa pamoja na jamaa yake Listra. Jina la mama yake ni Eunike na nyanya yake Loisi.

      Hii ndiyo mara ya tatu ya Paulo kutembelea Listra. Mwaka mmoja uliotangulia, Paulo na Barnaba walifika huku mara ya kwanza katika safari ya kuhubiri. Na sasa Paulo amerudi tena huko akiwa na rafiki yake Sila.

      Unajua Paulo anamwambia Timotheo nini? ‘Ungependa kwenda pamoja na Sila na mimi?’ anauliza. ‘Ungeweza kutusaidia kuhubiri watu wa mbali.’

      ‘Ndiyo,’ Timotheo ajibu, ‘ningependa kwenda.’ Basi upesi baada ya hapo Timotheo aacha jamaa yake na kwenda pamoja na Paulo na Sila.

  • Timotheo—Msaidizi Mpya wa Paulo
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
    • Timotheo anapokwenda na Paulo na Sila, unajua wanakwenda wapi? Angalia ramani, tujifunze sehemu chache.

      Ramani ya maeneo ambayo paulo na Timotheo walitembelea

      Kwanza, wanakwenda kwenye mji wa Ikonio, kisha mji wa pili wa Antiokia. Baada ya hapo wanasafiri kwenda Troʹa, kisha Filipi, Thesalonike na Beroya. Unaona Athene katika ramani? Paulo anahubiri huko. Kisha wanakaa mwaka mmoja na nusu wakihubiri Korintho. Mwishowe wanasimama kidogo katika Efeso. Kisha wanarudi Kaisaria kwa meli, na kusafiri kwenda juu Antiokia, ambako Paulo anakaa.

      Hivyo Timotheo anasafiri mamia na mamia ya kilomita akimsaidia Paulo azihubiri “habari njema” na kuanza makundi mengi ya Kikristo. Utakapokuwa mkubwa, je! utakuwa mtumishi mwaminifu wa Mungu kama Timotheo?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki