Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Via Egnatia—Barabara Kuu Iliyosaidia Kuleta Mpanuko
    Amkeni!—1997 | Agosti 22
    • [Ramani katika ukurasa wa 16, 17]

      (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

      UINGEREZA

      ULAYA

      AFRIKA

      BALKANI PENINSULA

      MAKEDONIA

      UGIRIKI

      Dirakiamu, Ilirikamu (DURRES, Albania)

      Thesalonike

      Apolonia

      Amfipolisi

      Filipi

      Neapolisi (Kaválla)

      Bizantiamu (Istanbul)

      BAHARI NYEUSI

      BAHARI YA MARMARA

      THRASI

      BAHARI YA AEGEAN

      Troasi

      UTURUKI

      [Hisani ya Picha katika ukurasa wa 16]

      Mountain High Maps® Copyright © 1995 Digital Wisdom, Inc.

  • Via Egnatia—Barabara Kuu Iliyosaidia Kuleta Mpanuko
    Amkeni!—1997 | Agosti 22
    • Via Egnatia—Barabara Kuu Iliyosaidia Kuleta Mpanuko

      NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA UGIRIKI

      KATIKA mwaka wa 50 W.K., kikundi cha wamishonari Wakristo kilikwenda kwa mara ya kwanza Ulaya. Walikuwa wamekuja kwa mwaliko uliopokewa na mtume Paulo katika maono: “Vuka uingie Makedonia utusaidie.” (Matendo 16:9) Ujumbe juu ya Yesu Kristo ambao Paulo na waandamani wake walileta ulikuwa na athari kubwa sana Ulaya.

      Msaada mkubwa sana katika kueneza Ukristo katika Makedonia ulikuwa Via Egnatia, barabara kuu ya Roma iliyotengenezwa. Baada ya kutua kwenye bandari ya Neapolisi (sasa Kaválla, Ugiriki) mwisho wa kaskazini mwa Bahari ya Aegean, wamishonari hao kwa wazi walisafiri kwenye barabara kuu hiyo hadi Filipi, jiji kuu la wilaya ya Makedonia. Barabara hiyo iliendelea hadi Amfipolisi, Apolonia, na Thesalonike, zilizokuwa sehemu ambazo Paulo angetua pamoja na waandamani wake.—Matendo 16:11–17:1.

  • Via Egnatia—Barabara Kuu Iliyosaidia Kuleta Mpanuko
    Amkeni!—1997 | Agosti 22
    • Baada ya kutua Neapolisi katika mwaka wa 50 W.K., mtume Paulo na waandamani wake walisafiri kilometa 16 kuelekea kaskazini-magharibi kwenye Via Egnatia hadi Filipi.

      “Siku ya sabato,” akaandika Luka, “tulitoka nje ya lango kando ya mto, ambako tulikuwa tukifikiri kulikuwako mahali pa sala; nasi tukaketi na kuanza kusema na wanawake waliokuwa wamekusanyika.” Miongoni mwa wanawake waliomsikiliza Paulo alikuwa Lidia. Siku hiyohiyo, yeye na nyumba yake wakawa waamini.—Matendo 16:13, 14.

      Kutoka Filipi, Paulo na washiriki wake waliendelea kwenye Via Egnatia kupitia Amfipolisi na Apolonia hadi Thesalonike, jumla ya kilometa 120. (Matendo 17:1)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki