-
Kujitahidi Kuwa WashindiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
7, 8. Kama vile kundi katika Smirna, kundi la Kikristo ‘lilitiwaje kenyekenye kwenye mtihani’ katika 1918?
7 Sawasawa na Wakristo katika Smirna, ile jamii ya Yohana na waandamani wao leo wamekuwa na wanaendelea “kutiwa kenyekenye kwenye mtihani.” Uaminifu wao chini ya jaribu huwatia alama ya kuwa watu wa Mungu mwenyewe. (Marko 13:9, 10) Muda mfupi baada ya siku ya Bwana kuanza, maneno ya Yesu kwa Wakristo katika Smirna yalileta faraja halisi kwa kikundi kidogo cha kimataifa cha watu wa Yehova. (Ufunuo 1:10) Tangu 1879, hao walikuwa wamekuwa wakichimbua kutoka Neno la Mungu utajiri wa kiroho ambao wao walishiriki na wengine bila malipo. Lakini wakati wa Vita ya Ulimwengu 1, walikutana na chuki na upinzani mkali, kwa sehemu kwa sababu wao hawakujitia katika ile harara ya vita na kwa sehemu kwa sababu wao walikuwa wakifunua wazi bila woga makosa ya Jumuiya ya Wakristo. Ule mnyanyaso ambao wao walipokea ukichochewa na baadhi ya viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo ulifikia upeo katika 1918 na ulilinganika na ule waliopokea Wakristo katika Smirna kutoka jamii ya Kiyahudi iliyokuwa huko.
8 Wimbi moja la mnyanyaso katika United States ya Amerika lilifikia upeo wakati yule msimamizi mpya wa Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi, Joseph F. Rutherford, na washiriki saba walipelekwa kwenye gereza katika Juni 22, 1918, walio wengi wao wakiwa na hukumu za kifungo cha miaka 20. Waliachiliwa kwa dhamana miezi tisa baadaye. Mei 14, 1919, mahakama ya rufani ilibadili hatia walizowekewa kimakosa; ilionyeshwa kulikuwako makosa 130 katika jaribio hilo. Jaji Manton, Mroma Katoliki, mwenye daraja la utawa wa Mtakatifu Gregori Mkuu, ambaye katika 1918 alikuwa amekataa dhamana kwa hao Wakristo, baadaye katika 1939, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na faini ya dola 10,000 kwa mashtaka sita ya kuomba na kupokea rushwa.
9. Mashahidi wa Yehova katika Ujeremani wa Nazi walitendwaje na Hitla, na kukiwa tendo-mwitikio gani kutoka viongozi wa kidini?
9 Wakati wa utawala wa Nazi katika Ujeremani, Hitla alipiga marufuku kabisa kabisa kazi ya kuhubiri ya Mashahidi wa Yehova. Kwa miaka kadhaa, maelfu ya Mashahidi walifungwa ndani ya kambi za mateso na magereza kikatili, ambako wengi walikufa, huku wanaume vijana 200 ambao walikataa kupigana katika jeshi la Hitla wakifishwa kwa amri ya serikali. Uungaji-mkono wa viongozi wa kidini wa yote haya unathibitishwa na maneno ya padri Mkatoliki, yaliyochapishwa katika ile nyusipepa The German Way ya Mei 29, 1938. Kwa sehemu, yeye alisema: “Sasa kuna nchi moja duniani ambako wale wanaoitwa eti . . . Wanafunzi wa Biblia [Mashahidi wa Yehova] wamekatazwa. Hiyo ni Ujeremani! . . . Wakati Adolf Hitla alipochukua mamlaka, nayo Episkopati ya Kikatoliki katika Ujeremani ikarudia ombi lao, Hitla akasema: ‘Hawa wanaoitwa eti Wanafunzi wa Biblia [Mashahidi wa Yehova] Wenye Bidii ni wafanyiza matata; . . . mimi nawaona kuwa wadanganyaji; mimi sivumilii kwamba Wakatoliki Wajeremani watatupiwa matope jinsi hiyo na huyu Mwamerika Jaji Rutherford. Mimi nafumua [Mashahidi wa Yehova] katika Ujeremani.’” Kwa hayo, yule padri akaongeza: “Hongera!”
10. (a) Kadiri ile siku ya Bwana imeendelea, Mashahidi wa Yehova wamekabili mnyanyaso gani? (b) Mara nyingi tokeo lilikuwa nini wakati Wakristo walipopigania uhuru wa kidini katika mahakama?
10 Kadiri ile siku ya Bwana imesonga mbele, yule Nyoka na mbegu yake hawakukoma kamwe kupiga vita dhidi ya Wakristo wapakwa-mafuta na waandamani wao. Wengi wa hawa wametiwa gerezani na kunyanyaswa kikatili sana. (Ufunuo 12:17) Maadui hao wameendelea ‘kutunga madhara kwa njia ya sheria,’ lakini watu wa Yehova kwa uthabiti husisitiza: “Ni lazima sisi tutii Mungu kuwa mtawala kuliko wanadamu.” (Zaburi 94:20; Matendo 5:29, NW) Katika 1954 gazeti Mnara wa Mlinzi liliripoti: “Zaidi ya nchi sabini katika wakati mmoja au mwingine katika muda wa miaka arobaini iliyopita zimefanyiza amri zuifu nazo zimenyanyasa Mashahidi wa Yehova.” Mahali ambako imewezekana kupigania uhuru wa kidini katika mahakama, Wakristo hawa wamefanya hivyo na katika nchi kadha wa kadha wamepata ushindi mwingi wenye mshindo mkubwa. Katika Mahakama Kuu Zaidi ya United States pekee, Mashahidi wa Yehova wameshinda maamuzi 50 yenye kupendeleka.
11. Ni unabii gani wa Yesu kuhusu ile ishara ya kuwapo kwake ambao umetimizwa juu ya Mashahidi wa Yehova wakati wa hii siku ya Bwana?
11 Hakuna kikundi kinginecho chote kimekuwa chenye kudhamiria kadiri hiyo katika kutii amri ya Yesu ya kulipa Kaisari vitu vya Kaisari. (Luka 20:25; Warumi 13:1, 7) Hata hivyo, hakuna kikundi kinginecho chote kimekuwa na washiriki waliotiwa gerezani katika mabara mengi hivyo chini ya namna nyingi hivyo mbalimbali za serikali, na jambo hili linaendelea mpaka wakati uu huu katika zile bara za Amerika, katika Europa, katika Afrika, na katika Esia. Unabii mkubwa wa Yesu kuhusu ile ishara ya kuwapo kwake ulitia ndani maneno haya: “Kisha watu watakabidhi nyinyi katika dhiki na wataua nyinyi, na nyinyi mtakuwa vitu vya kuchukiwa na mataifa yote kwa sababu ya jina langu.” (Mathayo 24:3, 9, NW) Bila shaka hilo limetimizwa juu ya Mashahidi Wakristo wa Yehova wakati wa hii siku ya Bwana.
12. Jamii ya Yohana imeimarishaje watu wa Mungu dhidi ya mnyanyaso?
12 Ili kuwaimarisha watu wa Mungu dhidi ya dhiki, ile jamii ya Yohana kwa kuendelea imewakumbusha maana ya maneno ya Yesu kwa Wakristo katika Smirna. Kwa mfano, mnyanyaso wa Kinazi ulipoanza, Mnara wa Mlinzi katika 1933 na 1934 ulikuwa na makala kama vile “Msiwaogope,” ambayo ilizungumzia Mathayo 10:26-33; “Lile Tanuri,” iliyotegemea Danieli 3:17, 18; na “Makanwa ya Simba,” Danieli 6:22 lilikuwa andiko kuu. Katika miaka ya muda wa tangu 1980, mwongo ambao katika huo kitabu hiki kilichapishwa kwa mara ya kwanza na Mashahidi wa Yehova wakanyanyaswa vikali katika mabara zaidi ya 40, Mnara wa Mlinzi uliimarisha watu wa Mungu kwa makala kama vile “Wenye Furaha Wajapoteswa!” na “Wakristo Wanaelekeana na Mateso kwa Uvumilivu.”b
13. Kama vile Wakristo katika Smirna, ni kwa nini Mashahidi Wakristo wa Yehova hawajakuwa wakiogopa mnyanyaso?
13 Kweli kweli, Mashahidi wa Yehova Wakristo wanapata mnyanyaso wa kimwili na mitihani mingine kwa siku kumi za mfano. Kama vile Wakristo huko nyuma katika Smirna, wao hawakuwa wakiogopa; wala hakuna yeyote wetu anayehitaji kuogopa taabu zizidipo kuwa mbaya hapa duniani. Sisi tuko tayari kuvumilia chini ya mateso na hata ‘kukubali kunyang’anywa mali zetu kwa furaha.’ (Waebrania 10:32-34) Kwa kujifunza Neno la Mungu na kulifanya liwe letu wenyewe, sisi tutatayarishwa tusimame tukiwa thabiti katika imani. Uwe na hakika kwamba Yehova anaweza kulinda na atalinda wewe katika ukamilifu wako. ‘Tupia yeye mahangaiko yako yote, kwa sababu yeye anakujali wewe.’—1 Petro 5:6-11, NW.
-
-
Kujitahidi Kuwa WashindiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 39]
Kwa miaka mingi, wanahistoria wamekuwa wakiandaa ushahidi kuhusu ukamilifu wa Mashahidi wa Yehova Wajeremani wakati wa utawala wa Nazi. Kitabu Mothers in the Fatherland, cha mwanahistoria Claudia Koonz, kilichochapishwa 1986, kinasema: “Idadi iliyo kubwa sana ya Wajeremani wote kutoka asili zisizo za Kinazi walipata njia za kuishi chini ya utawala waliodharau. . . . Kwenye ule upande mwingine wa spektra ya kitakwimu na ya kiitikadi walikuwako Mashahidi wa Yehova 20,000, ambao, karibu kila mmoja wao, walikataa katakata kutoa namna yoyote ya utii kwa serikali ya Nazi. . . . Kikundi chenye kushikamana zaidi ya vyote cha wakinzani kilitegemezwa na dini. Tangu mwanzo, Mashahidi wa Yehova hawakushirikiana na sehemu yoyote ya serikali ya Nazi. Hata baada ya Gestapo kuharibu makao makuu yao ya taifa katika 1933 na wakapiga marufuku farakano hilo katika 1935, wao walikataa kufanya jambo hata lililo dogo kama vile kusema ‘Heil Hitler.’ Wapatao nusu (zaidi wakiwa wanaume) wa Mashahidi wa Yehova wote walipelekwa kwenye kambi za mateso, elfu moja yao walifishwa, na elfu nyingine ikafa kati ya 1933 na 1945. . . . Wakatoliki na Waprotestanti walisikia viongozi wao wa kidini wakiwahimiza washirikiane na Hitla. Ikiwa wao walipinga, wao walifanya hivyo kinyume cha maagizo kutoka kwa kanisa na serikali pia.”
-
-
Kushikilia kwa Imara Jina la YesuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Katika United States, mamia ya watoto na walimu walifukuzwa shuleni kwa sababu hawakusalimu bendera ya kitaifa, hali katika Ujeremani Mashahidi walinyanyaswa vikali kwa kukataa kusalimu swastika. Kama ilivyokwisha kuonyeshwa, Wanazi wa Hitla waliua watumishi washikamanifu wa Yehova kwa sababu walikataa kushiriki ibada ya sanamu kama hiyo ya kitaifa. Katika miaka ya 1930, wakati wa usitawi mwingi wa ibada ya Shinto ya maliki wa Japani, wahudumu wawili mapainia walipanda mbegu nyingi za Ufalme katika Taiwani iliyokaliwa na Wajapani. Watawala wa kivita waliwatupa gerezani, ambamo mmoja wao alikufa kwa sababu ya kutendwa kikatili. Yule mwingine aliachiliwa baadaye, akaja tu kupigwa risasi mgongoni—Antipasi wa ki-siku-hizi. Mpaka leo hii, kuna mabara ambamo ibada ya mifano ya kitaifa na kujitoa kabisa kabisa kwenye serikali ni mambo yanayodaiwa. Mashahidi wengi vijana wametiwa gerezani, na si wachache wakafishwa, kwa sababu ya msimamo wao wa ushujaa wakiwa Wakristo wasiokuwamo. Ikiwa wewe ni kijana anayekabili masuala kama hayo, jifunze neno la Mungu kila siku ili wewe uweze ‘kuwa na imani ya kuhifadhi hai nafsi’ kwa kutazamia uhai wa milele.—Waebrania 10:39–11:1, NW; Mathayo 10:28-31.
7. Vijana wachanga katika India walikabilije suala la ibada ya utukuzo wa taifa, na kwa tokeo gani?
7 Walio wachanga wameelekeana na masuala kama hayo shuleni. Katika 1985 katika mkoa wa Kerala, India, watoto watatu wachanga wa Mashahidi wa Yehova walikataa kuacha msimamo wao uliotegemea imani ya Biblia, wakikataa kuimba wimbo wa kutukuza taifa. Wao walisimama kwa heshima huku wengine wakiimba, lakini hata hivyo walifukuzwa shuleni. Baba yao alikata rufani ya tendo hilo moja kwa moja mpaka Mahakama Kuu Zaidi ya India ambako majaji wawili waliamua kwa kupendelea watoto, wakitaarifu hivi kwa ujasiri: “Pokeo letu hufundisha uvumiliano, falsafa yetu hufundisha uvumiliano; katiba yetu huzoea uvumiliano; acheni sisi tusiipunguze nguvu.” Utangazaji wa nyusipepa na tahariri zenye kupendeleka zilizotokana na kesi hii zilijulisha taifa zima, ambalo wakati huo idadi yake ilikaribia sehemu moja kwa tano ya idadi ya dunia, kwamba kuna Wakristo katika bara lile ambao huabudu Mungu wa kweli Yehova na kwamba hawa wanasimama kishikamanifu kwa kanuni za Biblia.
-