Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nuru Yamalizia Enzi ya Giza
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Januari 15
    • Maisha ya Kiyahudi Katika Nyakati za Kiajemi

      Kufuatia tangazo la Sairasi lililowafungua Wayahudi kutoka utekwa wa Kibabiloni katika 537 K.W.K., kikundi cha Wayahudi na washiriki wao Wasio Wayahudi kiliondoka Babilonia. Mabaki hao walioitikia kiroho walirudi katika eneo la majiji yaliyoharibiwa na bara lililofanywa ukiwa. Waedomu, Wafoinike, Wasamaria, makabila ya Kiarabu, na wengineo walikuwa wamepunguza eneo la Israeli ambalo wakati mmoja lilikuwa kubwa. Kile kilichosalia kutoka Yuda na Benjamini kilikuja kuwa mkoa wa Yuda katika jimbo la Uajemi lililoitwa Abar Nahara (Ng’ambo ya Mto).—Ezra 1:1-4; 2:64, 65.

      Chini ya utawala wa Uajemi, Yuda ikaanza kupata “kipindi cha mpanuko na ukuzi wa idadi ya watu,” chasema The Cambridge History of Judaism. Chaendelea kusema hivi kuhusu Yerusalemu: “Wakulima na wapilgrimu walileta zawadi, Hekalu na jiji likawa tajiri, na utajiri walo ukavutia wafanyabiashara na mafundi.” Ingawa Waajemi waliruhusu sana serikali na dini ya hapo kufanya mambo, kodi ilikuwa kali sana na ilikuwa ilipwe kwa madini yenye thamani pekee.—Linganisha Nehemia 5:1-5, 15; 9:36, 37; 13:15, 16, 20.

      Miaka ya mwisho ya Milki ya Uajemi ilikuwa nyakati zenye msukosuko sana, ikiwa na maasi ya maliwali. Wayahudi wengi walijihusisha katika uasi mmoja kwenye Pwani ya Mediterania nao walihamishwa mbali kaskazini, kwenda Hyrcania kwenye Bahari ya Kaspiani. Hata hivyo, sehemu kubwa zaidi ya Yuda inaonekana haikuathiriwa na adhabu ya Uajemi.

  • Nuru Yamalizia Enzi ya Giza
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Januari 15
    • Katika miaka ya mapema ya baada ya kutoka uhamishoni, Wayahudi waaminifu walikinza kuchanganywa kwa mawazo na falsafa za kipagani na dini ya kweli iliyofunuliwa katika Maandiko ya Kiebrania. Kitabu cha Esta, kilichoandikwa baada ya zaidi ya miaka 60 ya ushirikiano wa karibu pamoja na Uajemi, hakina dalili yoyote ya Uzoroastria. Isitoshe, hakuna uvutano wa dini hii ya Kiajemi upatikanao katika vitabu vya Ezra, Nehemia, au Malaki, vyote vikiwa viliandikwa mapema katika enzi ya Kiajemi (537-443 K.W.K.).

      Hata hivyo, wasomi huamini kwamba katika sehemu ya mwisho ya enzi ya Kiajemi, Wayahudi wengi walianza kukubali baadhi ya maoni ya waabudu wa Ahura Mazda, mungu mkuu wa Waajemi. Hilo laonwa katika ushirikina wenye kupendwa na itikadi za Waesene. Maneno ya kawaida ya Kiebrania ya mbweha, viumbe vingine vya jangwa, na ndege wa usiku yakaja kushirikishwa katika akili za Kiyahudi na roho waovu na madubwana wa usiku wa hadithi za Kibabiloni na Kiajemi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki