-
Unamna-Namna wa Viumbe Katika Msitu wa AmazoniAmkeni!—2010 | Aprili
-
-
Tamaduni Zahitilafiana
Katika karne za 16 na 17, Wahispania walivamia msitu wa Amazoni. Muda mfupi baadaye, wamishonari Wajesuti na wale wa Mtakatifu Francis walifika wakiwa na nia ya kuwabadili wenyeji wawe Wakatoliki. Wamishonari hao walichora ramani kwa ustadi zilizofanya wakazi wa Ulaya waufahamu vizuri msitu huo wa Amazoni. Lakini pia wamishonari hao walileta magonjwa na uharibifu katika msitu huo.
Kwa mfano, mwaka wa 1638 walianzisha kituo cha Kikatoliki katika eneo linalojulikana sasa kama Mkoa wa Maynas. Wamishonari waliwakusanya wenyeji na kuwalazimisha kuishi pamoja kama jamii, hata makabila yaliyokuwa na uhasama. Kwa kusudi gani? Kwa kuwa wenyeji walionwa kuwa wasio na akili na watu wa hali ya chini, walilazimishwa kuwafanyia kazi wamishonari na Wahispania waliokuwa wakoloni. Kwa sababu ya kuishi kwa ukaribu na watu hao kutoka Ulaya, maelfu ya wenyeji walikufa kutokana na surua, ndui, dondakoo, na ukoma. Maelfu ya wengine walikufa kwa sababu ya njaa.
Wenyeji wengi wa Asili wa Amerika walitoroka kambi zilizokuwa zimeanzishwa na vikundi mbalimbali vya kidini na wamishonari wengi waliuawa wakati wa ghasia. Wakati mmoja katika miaka ya mapema ya karne ya 19, ni kasisi mmoja tu aliyebaki katika eneo la Amazoni.
-
-
Unamna-Namna wa Viumbe Katika Msitu wa AmazoniAmkeni!—2010 | Aprili
-
-
Kutawaliwa na Waganga na Ushirikina
Wakazi wa msitu wa Amazoni huamini kwamba msitu huo umejaa nafsi zinazozurura usiku, roho zinazosababisha magonjwa, na miungu inayojificha ndani ya mito ikisubiri kuwanasa watu. Fikiria kuhusu Aguaruna, moja kati ya makabila makubwa zaidi nchini Peru. Wanaabudu miungu mitano tofauti: “Baba Shujaa wa Vita,” “Baba wa Maji,” “Mama wa Dunia,” “Baba wa Jua,” na “Baba wa uganga.” Wengi wanaamini kwamba wanadamu wanabadilishwa kuwa mimea na wanyama. Kwa kuwa wanaogopa kuwakasirisha viumbe wa roho, wenyeji huepuka kuwaua wanyama fulani nao huwawinda wengine inapohitajika tu.
Waganga ndio husimamia maisha ya kidini na ya kijamii. Wao hutumia mimea kujipumbaza akili. Watu fulani katika maeneo hayo huwatazamia waganga hao watibu magonjwa, watabiri jinsi uwindaji na mavuno yatakavyokuwa, na kutabiri matukio ya wakati ujao.
-