Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Moyo Wangu Wafurika kwa Shukrani
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 1
    • Mwaka huo pia niliwekwa kuwa mtumishi wa vikuza-sauti. Siku hizo tulitumia mashine ya kupigia sahani za santuri iliyovumisha hadharani ujumbe “Dini Ni Mtego na Hila.” Wakati huo mkazo ulitiwa juu ya kufichua unafiki na mafundisho yasiyo ya kweli ya Jumuiya ya Wakristo.

  • Moyo Wangu Wafurika kwa Shukrani
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 1
    • Kwa upande mwingine, mashine yetu ya kupigia sahani za santuri (ambayo ilikuwa inaweza kutumiwa kwa wasikilizaji wengi zaidi) ilikuwa nzito zaidi, na tuliibeba katika kigari au gari la kubeba mtoto mchanga.

  • Moyo Wangu Wafurika kwa Shukrani
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 1
    • Tulipokuwa Swansea, South Wales, mwenzangu, Don Rendell, hakuachiliwa asifanye utumishi wa kijeshi. Alitiwa gerezani licha ya kueleza kwamba hangaliweza kwa kudhamiria kupigana dhidi ya Wakristo wenzake katika nchi nyingine. (Isaya 2:2-4; Yohana 13:34, 35) Ili kumtia moyo, na vilevile kuwatolea majirani ushahidi, niliweka ile mashine ya kupigia sahani za santuri karibu na gereza na kucheza hotuba za Biblia.

      Hata hivyo, wanawake wa mahali hapo walichukizwa na jambo hilo na walipitisha kofia ya kukusanya pesa ili kuwalipa askari wapige mwandamani wangu na mimi. Tuliondoka, tukikimbia kadiri tulivyoweza—nilikuwa pia nikisukuma kile kigari chenye mashine ya kupigia sahani za santuri—tukitafuta kinga ya Jumba la Ufalme. Lakini tulipofika hapo, lilikuwa limefungwa! Kuingilia kati tu kwa polisi wakati ufaao ndiko kulikotuokoa tusipigwe vikali.

      Kwa wazi tukio hilo likaja kujulikana sana. Nilipokuwa nikihubiri katika nchi iliyo karibu na Swansea muda fulani baadaye, mtu fulani aliniambia hivi kwa kibali: “Ukristo ni jambo lile mnalotetea, kama yule mwanamume kijana katika Swansea aliyetangaza kwa ujasiri alichoamini na kulazimika kukimbilia kinga.” Alishangaa kama nini kujua kwamba mimi nilikuwa ndiye yule mwanamume kijana!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki