Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kazi Iliyofanywa kwa Ustadi Mkubwa Sana”
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Januari 15
    • Muda si muda kulikuwa na seti za “Eureka Drama” mbali na ile drama ya kawaida ya “Photo-Drama of Creation.” (Ona sanduku.) Seti moja ilikuwa imefanyizwa kwa hotuba na vilevile muziki uliorekodiwa. Seti ile nyingine ilifanyizwa kwa rekodi na kwa slaidi pia. Ingawa “Eureka Drama” haikuwa na picha kama za sinema, ilikuwa na matokeo sana ilipoonyeshwa katika maeneo yasiyokuwa na watu wengi.

  • “Kazi Iliyofanywa kwa Ustadi Mkubwa Sana”
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Januari 15
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 8, 9]

      “Eureka Drama”

      Miezi minane baada ya “Photo-Drama” kuonyeshwa kwa mara ya kwanza, Sosaiti iliona uhitaji wa kutoa aina nyingine ya drama iitwayo “Eureka Drama.” Japo “Photo-Drama” iliyokuwa kamili iliendelea kuonyeshwa katika majiji makubwa, seti za “Eureka” zilitoa ujumbe ule ule wa msingi vijijini na mashambani. Aina moja ya “Eureka Drama” ilisemwa kuwa iliwapa “akina dada fursa ya pekee” ya kuhubiri. Kwa nini? Kwa sababu sanduku lake la rekodi za santuri lilikuwa na uzito wa kilogramu 14 pekee. Bila shaka, ingekuwa lazima kubeba kinanda cha santuri kwa ajili ya maonyesho.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki