-
Mwaka wa Kipekee wa EinsteinAmkeni!—2005 | Septemba 8
-
-
Kuvumbua Siri za Nuru
Hati ya Einstein iliyochapishwa Machi 1905, ilifichua siri fulani kuhusu nuru. Tayari wanasayansi walikuwa wamegundua kwamba nuru inaposafiri angani, hufanana na viwimbi vya maji katika kidimbwi. Hata hivyo, nadharia ya mawimbi haingeweza kueleza sababu inayofanya nuru ya buluu hafifu itokeze mkondo wa umeme inapogonga metali fulani, huku nuru nyekundu nyangavu ikose kufanya hivyo. Hati ya Einstein ilisaidia kueleza ile inayoitwa athari ya umeme-nuru.
Einstein alidai kwamba nyakati nyingine nuru inaweza kuonwa kuwa imefanyizwa kwa kiasi kidogo cha nguvu ambacho baadaye kiliitwa fotoni. Fotoni hizo zinapokuwa na kiasi kilekile cha nguvu au rangi, zinaweza kufanya elektroni za metali fulani zitengane na atomu zake. (Fotoni za nuru nyekundu haziwezi kufanya hivyo kwa kuwa ni hafifu sana.) Muungano huo hutokeza mkondo wa umeme katika metali. Vitu vilivyovumbuliwa karibuni kama vile neli za televisheni za kutokeza picha, betri za jua, na vifaa vya kupima nuru, vilibuniwa kulingana na maelezo ya Einstein kuhusu athari ya umeme-nuru.
Einstein alishinda Tuzo ya Nobeli ya Fizikia ya mwaka wa 1921 kwa sababu ya ufafanuzi wake kuhusu nuru. Hati yake ilichangia kuanzishwa kwa nyanja mpya ya sayansi iliyoitwa nadharia ya kwanta. Kwa sababu ya hilo, nadharia ya kwanta ikawa msingi wa kuvumbua mambo mengine mengi kutia ndani sayansi ya nyuklia, elektroniki, na nanotechnology.
-
-
Mwaka wa Kipekee wa EinsteinAmkeni!—2005 | Septemba 8
-
-
[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 20]
(See publication)
Nuru hutenda kama viwimbi na pia kama chembechembe. Kuelewa jambo hilo kumefanya iwezekane kuwa na vifaa vya kufanyia hesabu vinavyotumia jua, na vifaa vya kunasa nuru katika kamera zinazotumia kompyuta
-