-
“Hakuna Aliye na Upendo Mkuu Kuliko Huu”‘Njoo Uwe Mfuasi Wangu’
-
-
1-4. (a) Umati wenye hasira uliokusanyika nje ya jumba la gavana unafanya nini Pilato anapomleta Yesu? (b) Yesu anafanya nini anapoaibishwa na kuteswa, na ni maswali gani tunayopaswa kufikiria kwa uzito?
“TAZAMENI! Mwanamume!” Gavana Mroma Pontio Pilato anasema maneno hayo anapomleta Yesu Kristo kwenye umati wenye hasira uliokusanyika nje ya jumba la gavana wakati wa mapambazuko, siku ya Pasaka ya mwaka wa 33 W.K. (Yohana 19:5) Siku chache tu mapema, umati huo ulimsifu Yesu alipoingia Yerusalemu kwa shangwe ya ushindi akiwa Mfalme aliyewekwa na Mungu. Hata hivyo, usiku huu, umati huo wenye chuki unamwona kwa njia tofauti kabisa.
2 Yesu amevikwa vazi la zambarau kama la wafalme, na ana taji kichwani. Hata hivyo, kuvikwa kwake vazi hilo, linaloufunika mgongo wake unaotoka damu kwa sababu ya kupigwa mijeledi, na taji, lililotengenezwa kwa miiba na kushindiliwa kwenye kichwa chake kinachotoka damu, ni njia ya kudhihaki cheo chake cha kifalme. Watu wakiwa wamechochewa na wakuu wa makuhani, wanamkataa mwanamume aliyepigwa aliye mbele yao. Makuhani wanapaaza sauti hivi: “Mtundike mtini! Mtundike mtini!” Wakitaka sana auawe, wanapiga kelele wakisema: “Anapaswa kufa.”—Yohana 19:1-7.
3 Yesu anavumilia aibu zote hizo na mateso hayo kwa uhodari na bila kunung’unika.a Yuko tayari kabisa kufa.
-