-
Matukio Muhimu ya Mwaka Uliopita2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Ureno
Septemba 25, 2009 (25/9/2009), Wizara ya Haki ilisema kwamba shirika la Association of Jehovah’s Witnesses limeidhinishwa bila kupingwa kuwa Jamii ya Kidini Ambayo Imekuwepo kwa Muda Mrefu. Sasa Mashahidi wa Yehova nchini Ureno wamepewa usajili wa juu zaidi kisheria na kidini, na hilo litawasaidia sana kutimiza huduma yao. Msimamo wao mpya wa kisheria utawapa watu wa Yehova faida nyingi. Zinatia ndani kuwa na wahudumu waliowekwa rasmi kuandikisha ndoa kisheria katika Majumba ya Ufalme na vilevile mamlaka ya kuingia hospitalini na gerezani kuwapa watu wowote wanaotaka msaada wa kiroho.
-
-
Matukio Muhimu ya Mwaka Uliopita2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 25]
Cheti kilichotolewa na Wizara ya Haki
-