Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kufanya Mimba Yako Iwe Salama Zaidi
    Amkeni!—2003 | Januari 8
    • Ulaji. Kulingana na Muungano wa Matokeo Bora ya Uzazi, mwanamke anahitaji angalau miezi minne kabla ya kuwa na mimba baada ya kufanya kazi karibu na bidhaa zinazodhuru, ili pia apate kuwa na afya bora. Kwa mfano, hatari ya kupinda uti wa mgongo inayoletwa na kutoziba kwa mrija wa neva wa kitoto kilicho tumboni, inaweza kuzuiwa iwapo mama mjamzito ana kiasi cha kutosha cha aina fulani ya vitamini ya C. Kwa kuwa mrija huo huziba siku ya 24 hadi ya 28 baada ya mimba kutungwa—muda mrefu kabla ya wanawake wengi kugundua wana mimba—baadhi ya wanawake wanaopanga kupata mimba hula vyakula vyenye vitamini hiyo.

      Chuma ni madini muhimu pia. Kwa hakika, mwanamke huhitaji madini mengi zaidi ya chuma anapokuwa mjamzito. Asipokuwa na kiasi cha kutosha—hali ambayo huwapata wanawake wengi katika nchi zinazoendelea—damu yake inaweza kuwa na upungufu wa madini hayo. Hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi mwanamke apatapo mimba moja baada ya nyingine, kwa kuwa hana nafasi ya kurudisha kiasi kinachohitajika cha madini ya chuma.a

  • Kufanya Mimba Yako Iwe Salama Zaidi
    Amkeni!—2003 | Januari 8
    • [Sanduku katika ukurasa wa 14]

      MADOKEZO YA KUWASAIDIA WANAWAKE WAJAWAZITO

      ● Kila siku mwanamke mjamzito anahitaji kula matunda, mboga (hasa zilizo na majani ya rangi nzito ya kijani, na zenye rangi ya machungwa, au nyekundu), maharagwe mbalimbali (kutia ndani soya, dengu, na njegere), nafaka (kutia ndani ngano, mahindi na shayiri—hasa zile ambazo hazijatolewa maganda au zilizotiwa vitu vingine), chakula kinachotokana na wanyama (samaki, nyama ya kuku, nyama ya ng’ombe, mayai, jibini, na maziwa, hasa yale ambayo yametolewa mafuta). Mafuta, sukari na chumvi vinapaswa kutumiwa kwa kiasi. Kunywa maji mengi. Epuka vinywaji vyenye kafeini, na vyakula vilivyotiwa dawa za kuhifadhi na kemikali nyinginezo (kama za kutia rangi na ladha). Wanga, udongo wa mfinyanzi, na vitu vingine visivyoliwa vyaweza kusababisha utapiamlo na kumtia sumu.

  • Kufanya Mimba Yako Iwe Salama Zaidi
    Amkeni!—2003 | Januari 8
    • Kuongeza uzito. Mwanamke mjamzito anapaswa kuepuka kupita kiasi katika ulaji. Kulingana na kichapo Krause’s Food, Nutrition and Diet Therapy, mtoto anayezaliwa akiwa na uzito wa chini sana anakabili hatari ya kufa mara 40 zaidi kuliko yule aliyezaliwa akiwa na uzito wa kawaida. Kwa upande mwingine, kula chakula cha watu wawili hunenepesha tu. Ongezeko linalofaa la uzito—ambalo huanza kuonekana katika mwezi wa nne wa mimba na kuendelea—huonyesha kwamba mama anakula chakula cha kutosheleza mahitaji yake yanayoongezeka.b

  • Kufanya Mimba Yako Iwe Salama Zaidi
    Amkeni!—2003 | Januari 8
    • a Aina hiyo ya vitamini ya C na madini ya chuma yaweza kupatikana katika maini, maharagwe, mboga zenye majani mabichi, njugu, na nafaka zilizoongezwa vitamini na madini mbalimbali. Kuchanganya chakula chenye vitamini ya C, kama matunda yaliyotoka shambani karibuni, pamoja na chakula chenye madini ya chuma huongeza madini hayo mwilini.

      b Ongezeko linalopendekezwa kwa mwanamke mwenye uzito unaofaa anapokuwa na mimba ni kilogramu 9 hadi 12 kufikia wakati wa kujifungua. Hata hivyo, wasichana au wanawake ambao hawakuwa wakila chakula cha kutosha wanapaswa kuongeza kati ya kilogramu 12 hadi 15, na wale wanene wanapaswa kuongeza kilogramu 7 hadi 9 tu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki