-
Mama Wenye Afya, Watoto Wenye AfyaAmkeni!—2009 | Novemba
-
-
[Blabu katika ukurasa wa 27]
Kulingana na tarakimu zilizochapishwa mnamo Oktoba 2007, mwanamke mmoja hufa karibu kila dakika, yaani, wanawake 536,000 kwa mwaka, kwa sababu ya matatizo yanayohusianishwa na uja-uzito.—Hazina ya Idadi ya Watu ya Umoja wa Mataifa
-
-
Mama Wenye Afya, Watoto Wenye AfyaAmkeni!—2009 | Novemba
-
-
Likizungumza kuhusu matatizo yanayoweza kuwakumba akina mama, jarida Journal of the American Medical Women’s Association linasema kwamba “sababu kuu zinazowafanya akina mama wengi wafe wanapojifungua” ni kuvuja damu nyingi, mtoto kukaa vibaya tumboni, maambukizo, na kupanda sana kwa shinikizo la damu. Hata hivyo, matibabu yanayofanya kazi yanajulikana sana na katika visa vingi “matibabu ya kisasa . . . hayahitaji matumizi ya vifaa tata,” linasema jarida hilo.
-