Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Siku ya Wageni Yenye Kusudi
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Novemba 1
    • Watu wengi walipendezwa na mashini ya uchapishaji inayoitwa MAN Roland Lithoman inayoweza kuchapisha magazeti 90,000 kwa saa. Pia wageni walivutiwa na eneo kubwa la upakiaji na usafirishaji linaloshughulikia vichapo zaidi ya tani 14 kila siku na vilevile wakavutiwa na eneo la kujalidi vitabu. Mashahidi katika idara mbalimbali walitayarisha vibao vya maonyesho, kutia ndani kimoja kilichoonyesha kwa ufupi historia ya uchapishaji, kuanzia na mashini za Gutenberg hadi zile za kisasa. Ubao mwingine ulionyesha jinsi ofisi ya tawi inavyotunza mazingira. Kwa mfano, sehemu fulani ya pekee inaondoa gesi zenye sumu na harufu kutoka kwenye mashini za uchapishaji, na vichujio vinakusanya vumbi linalotoka kwenye karatasi.

  • Siku ya Wageni Yenye Kusudi
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Novemba 1
    • Wageni wengi walithamini sana kutembelea ofisi hiyo na walishangaa kwamba ofisi hiyo ina vichapo vinavyotegemea Biblia katika lugha 151 na inachapisha vichapo kwa ajili ya nchi 18 kusini mwa Afrika na Afrika ya kati.

  • Siku ya Wageni Yenye Kusudi
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Novemba 1
    • [Picha katika ukurasa wa 15]

      Mashini ya MAN Roland Lithoman

      [Picha katika ukurasa wa 15]

      Mashini ya kujalidi vitabu

      [Picha katika ukurasa wa 15]

      Idara ya upakiaji na usafirishaji

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki