-
Matukio Muhimu Ya Mwaka Uliopita2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
Walipoidhinisha mpango huo mpya wa uchapaji, Baraza Linaloongoza pia liliidhinisha ununuzi wa matbaa saba kubwa sana za kuchapa aina ya MAN Roland Lithoman. Matbaa hizo mpya zina uwezo mkubwa kuliko zile za zamani, hivyo, zitatosheleza mahitaji ya wakati ujao. Tano kati ya matbaa hizo ni za ofisi ya tawi ya Afrika Kusini, Brazili, Japani, Mexico, na Uingereza, na tayari baadhi yake zimewekwa. Zile nyingine mbili ni za kiwanda cha Wallkill, New York, na imepangwa ziwekwe Aprili na Mei 2004. Kila matbaa ina urefu wa meta 40, inaweza kuchapa visehemu vya vitabu vyenye ukubwa wa gazeti, au magazeti, 90,000 kwa saa (25 kwa sekunde), na inaweza kuchapa kwa rangi pande zote mbili za karatasi kwa wakati mmoja.
-
-
Matukio Muhimu Ya Mwaka Uliopita2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
-
-
[Picha katika ukurasa wa 22, 23]
Matbaa ya kuchapa ikilinganishwa na basi
Ukubwa wa matbaa ya kuchapa:
Urefu: meta 41
Kimo: meta 5.5
Uzani: tani 201
-