Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Israeli Katika Siku Za Daudi Na Sulemani
    ‘Ona Nchi Nzuri’
    • Israeli Katika Siku Za Daudi Na Sulemani

      MUNGU aliahidi kuupatia uzao wa Abramu nchi ‘iliyotoka mto wa Misri mpaka mto Efrati.’ (Mwa 15:18; Kut 23:31; Kum 1:7, 8; 11:24) Baada ya Yoshua kuingia Kanaani, ilichukua muda wa karne nne hivi kwa Nchi ya Ahadi kufikia mipaka hiyo.

      Mfalme Daudi aliwashinda Waaramu waliotawala ufalme wa Soba ambao ulienea hadi Mto Efrati kaskazini mwa Siria.a Daudi alipowashinda Wafilisti, alipanua miliki yake upande wa kusini hadi kufikia mpaka wa Misri.—2Sa 8:3; 1Nya 18:1-3; 20:4-8; 2Nya 9:26.

      Mipaka (Wakati wa Sulemani)
      Daudi na Sulemani (barabara)

      Naye Sulemani alitawala “kutoka ule Mto [Efrati] hadi kwenye nchi ya Wafilisti na hadi kwenye mpaka wa Misri.” Utawala wake ulifananisha utawala wenye amani wa Mesiya. (1Fa 4:21-25; 8:65; 1Nya 13:5; Zb 72:8; Zek 9:10) Hata hivyo, inasemekana kwamba eneo lililokaliwa na Waisraeli ‘lilianzia Dani mpaka Beer-sheba.’—2Sa 3:10; 2Nya 30:5.

  • Israeli Katika Siku Za Daudi Na Sulemani
    ‘Ona Nchi Nzuri’
    • a Eneo la wana wa Rubeni lilifika kwenye Jangwa la Siria, na mpaka wake wa mashariki ulifika Mto Efrati.—1Nya 5:9, 10.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki