-
Sababu Tupo HapaAmkeni!—2008 | Desemba
-
-
Sababu Tupo Hapa
BIBLIA inaonyesha kwamba Muumba wetu, Yehova Mungu, hatendi bila kusudi. Kwa mfano, fikiria uumbaji wake wa mzunguko wa maji unaoendeleza uhai duniani. Biblia inaufafanua hivi kwa usahihi: “Mito yote hutiririkia baharini, lakini bahari kamwe haijai; huko ambako mito hutiririkia ndiko huko inakotoka tena.”—Mhubiri 1:7, Biblia Habari Njema.
Biblia inalinganisha kutegemeka kwa ahadi za Mungu na mzunguko ambao umefafanuliwa. Kama tunavyojua leo, nguvu za jua hufanya maji yavukizwe kutoka katika bahari na maziwa, na baadaye yanarudi duniani kama mvua. Yehova anaelekeza fikira kwenye mzunguko huo na kueleza: “Ndivyo litakavyokuwa neno langu linalotoka katika kinywa changu. Halitarudi kwangu bila matokeo, bali hakika litatenda yale ambayo yamenipendeza, na hakika litafanikiwa katika yale ambayo nimelituma.”—Isaya 55:10, 11.
-
-
Sababu Tupo HapaAmkeni!—2008 | Desemba
-
-
[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 7]
Biblia inalinganisha kutegemeka kwa ahadi za Mungu na mzunguko wa maji wenye kustaajabisha
[Mchoro]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Mvua
Uvukizaji
Uvukizaji
Maziwa, Mto
Bahari
-