-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
15. Ni wafalme gani wawili wenye nguvu waliotokana na falme nne za Kigiriki, nao walianzisha ushindani gani?
15 Kwa hiyo, wafalme wawili wenye nguvu—Niketa Seleuko wa Kwanza aliyetawala Siria na Ptolemy wa Kwanza aliyetawala Misri—waliibuka wakiwa wafalme wawili wenye nguvu kutokana na zile falme nne za Kigiriki. Ushindani wa muda mrefu unaofafanuliwa katika Danieli sura ya 11 kati ya “mfalme wa kaskazini” na “mfalme wa kusini,” ulianzishwa na wafalme hao wawili.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
“Mfalme wa kusini atakuwa hodari, na mmoja wa wakuu wake [wa Aleksanda]; naye [mfalme wa kaskazini] atakuwa hodari kuliko yeye, naye atakuwa na mamlaka; mamlaka yake itakuwa mamlaka kubwa.” (Danieli 11:5) Majina “mfalme wa kaskazini” na “mfalme wa kusini” yarejezea wafalme walio kaskazini na kusini mwa watu wa Danieli, ambao wakati huo walikuwa wamewekwa huru kutokana na utekwa wa Babiloni na walikuwa wamerudi Yuda. “Mfalme wa kusini” wa kwanza alikuwa Ptolemy wa Kwanza wa Misri.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
17. Mwanzoni mwa pambano kati ya mfalme wa kaskazini na mfalme wa kusini, Yuda ilitawalwa na nani?
17 Mwanzoni mwa pambano, Yuda ilikuwa ikitawalwa na mfalme wa kusini. Kuanzia mwaka wa 320 K.W.K. hivi, Ptolemy wa Kwanza aliwachochea Wayahudi waende wakae Misri. Jumuiya ya Kiyahudi ikasitawi Aleksandria, ambapo Ptolemy wa Kwanza alianzisha maktaba maarufu. Mfalme wa kusini, Misri iliyokuwa ikitawalwa na nasaba ya Ptolemy, aliendelea kutawala Wayahudi huko Yuda hadi mwaka wa 198 K.W.K.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
[Picha katika ukurasa wa 218]
Ptolemy wa kwanza
-