-
Makaburi Hutufunulia Imani za KaleAmkeni!—2005 | Desemba 8
-
-
Kuna magofu ya jiji la kale la Teotihuacán huko kaskazini-mashariki ya Mexico City. Jiji hilo lilikuwa na barabara iliyoitwa Barabara ya Wafu. Bahn aliyenukuliwa mapema anaandika hivi: “Baadhi ya sanamu kuu zaidi za ukumbusho ulimwenguni ziko kwenye barabara hiyo.” Sanamu hizo zinatia ndani Piramidi ya Jua na Piramidi ya Mwezi, ambazo zilijengwa katika karne ya kwanza W.K., na magofu ya Hekalu la Quetzalcoatl.
Inaonekana kwamba sehemu ya ndani ya Piramidi ya Jua ilikuwa mahali pa kuzikia watu wenye vyeo, labda kutia ndani makuhani. Mabaki ya binadamu yaliyopatikana katika makaburi ya ujumla yaliyo karibu yanadokeza kwamba huenda wapiganaji walitolewa kama dhabihu ili kulinda wale waliokuwa ndani. Mitindo tofauti-tofauti ya kuzika watu imefanya waakiolojia waamini kwamba eneo hilo lina mabaki ya watu 200 hivi, kutia ndani watoto ambao huenda walitolewa kama dhabihu katika programu ya kuzindua sanamu za ukumbusho.
-
-
Makaburi Hutufunulia Imani za KaleAmkeni!—2005 | Desemba 8
-
-
[Picha katika ukurasa wa 23]
Piramidi ya Jua na Barabara ya Wafu huko Teotihuacan, Mexico
[Hisani]
Top: © Philip Baird www.anthroarcheart.org; painting: Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.
-