-
“Fulizeni Kulinda”Mnara wa Mlinzi—2000 | Januari 15
-
-
18. Inaonekana hali itakuwaje kwa baadhi ya watiwa-mafuta wakati dhiki kubwa izukapo, na twaweza kujuaje jambo hilo?
18 Sababu ya sita, idadi ya wanafunzi wa kweli wa Kristo ambao ni watiwa-mafuta inapungua, ingawa yaonekana wengine wangali watakuwa duniani dhiki kubwa ianzapo. Wengi wa mabaki wamezeeka sana, na katika miaka ambayo imepita idadi ya wale ambao kwa kweli wametiwa mafuta inazidi kupungua. Lakini akirejezea dhiki kubwa, Yesu alisema: “Kama siku hizo hazingekatwa ziwe fupi, hakuna mwili ambao ungeokolewa; lakini kwa sababu ya wale wachaguliwa siku hizo zitakatwa ziwe fupi.” (Mathayo 24:21, 22) Kwa hiyo, inaonekana baadhi ya “wale wachaguliwa” wa Kristo watakuwako duniani dhiki kubwa izukapo.f
-
-
“Fulizeni Kulinda”Mnara wa Mlinzi—2000 | Januari 15
-
-
f Katika ule mfano wa kondoo na mbuzi, Mwana wa binadamu awasili katika utukufu wake wakati wa ile dhiki kubwa na kuketi ili kuhukumu. Kristo awahukumu watu kwa msingi wa kama walitegemeza ndugu zake watiwa-mafuta. Msingi huo wa kuhukumu haungekuwa na maana yoyote ikiwa wakati wa hukumu hiyo, ndugu wote wa Kristo wangekuwa tayari wameondoka duniani muda mrefu awali.—Mathayo 25:31-46.
-