Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Réunion
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Muda si mrefu, walipata watu wengi wenye kupendezwa na hata walifanya mikutano kwenye chumba chao hotelini katika jiji kuu la Saint-Denis. Mara tu familia hiyo ilipohamia nyumba nyingine, walianza kufanya mikutano huko. Mwaka mmoja hivi baadaye, ndugu katika kikundi hicho kipya jijini Saint-Denis walikodi ukumbi mdogo uliotoshea watu 30 hivi. Ukumbi huo uliojengwa kwa mbao na kuezekwa kwa mabati, ulikuwa na madirisha mawili na mlango mmoja. Baada ya kupata kibali, ndugu walibomoa kuta za ndani, wakajenga jukwaa dogo, na kuweka viti visivyo na sehemu ya kuegemea.

      Siku za Jumapili wakati jua lilipowaka asubuhi, paa hilo la mabati lilifanya ukumbi huo uwe na joto jingi. Baada ya muda, wote waliokuwa ndani walitokwa na jasho, hasa wale waliosimama jukwaani, vichwa vyao vikiwa karibu na paa. Isitoshe, kwa kuwa mara nyingi ukumbi huo ulijaa kabisa, watu wengi walisikiliza wakiwa kwenye madirisha na mlango, na kufanya waliokuwa ukumbini wakose hewa safi.

      “TUMELEMEWA KIDOGO!”

      Ingawa hali hiyo ilikuwa ngumu, wote walikaribishwa vizuri mikutanoni, na mwishoni mwa mwaka wa 1961 watu 50 hivi walihudhuria mikutano kwa ukawaida.

  • Réunion
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Watu waliohudhuria mikutano ya Jumapili waliongezeka hadi 100, nao walitoka jamii mbalimbali.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki