-
Ujumbe Mtamu na MchunguUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na yeye [huyo malaika] akapiga kilio kwa sauti kubwa kama vile wakati simba anaponguruma. Na wakati yeye alipopiga kilio kikuu, ngurumo saba zikatamka sauti zazo zenyewe.” (Ufunuo 10:3, NW)
-
-
Ujumbe Mtamu na MchunguUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
8. Ni nini zilizo ‘sauti za ngurumo saba’?
8 Wakati uliotangulia Yohana amesikia sauti zikitoka katika kiti cha ufalme chenyewe cha Yehova. (Ufunuo 4:5) Huko nyuma katika siku ya Daudi, nyakati nyingine ngurumo halisi ilikuwa ikisemwa kuwa ni “sauti ya Yehova.” (Zaburi 29:3, NW) Wakati Yehova alipotangaza kwa sauti yenye kusikika kusudi lake la kutukuza jina lake mwenyewe katika siku za huduma ya kidunia ya Yesu, kwa wengi ilisikika kama ngurumo. (Yohana 12:28, 29) Kwa sababu hiyo, inapatana na akili nzuri kukata maneno kwamba ‘zile sauti za ngurumo saba’ ni tamko la Yehova mwenyewe la makusudi yake. Uhakika wa kwamba kulikuwa na ngurumo saba hudokeza ukamili wa yale ambayo Yohana alisikia.
-