Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yohana Aona Yesu Aliyetukuzwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • ‘Unachoona andika katika hati-kunjo na kuipeleka kwenye makundi saba, katika Efeso na katika Smirna na katika Pargamamu na katika Thiatira na katika Sardisi na katika Filadelfia na katika Laodikia.’” (Ufunuo 1:10b, 11) Sauti yenye mamlaka na yenye kuamrisha kama ya tarumbeta, inamwambia Yohana aandikie “makundi saba.” Yeye atapokea mfululizo wa jumbe na kutangaza vitu atakavyoona na kusikia. Angalia kwamba yale makundi yanayotajwa hapa yalikuwako kikweli katika siku ya Yohana. Yote yalikuwa katika Esia Ndogo, ng’ambo tu ya bahari kutoka Patmosi. Yalikuwa yenye kuwasilikana kwa urahisi yenyewe kwa yenyewe kwa njia ya barabara bora zaidi za Kiroma zilizokuwako katika eneo hilo. Mjumbe hangalipata shida ya kupeleka hati-kunjo kutoka kundi moja kwenda lifuatalo. Makundi saba haya yangelingana na sehemu ya mzunguko wa ki-siku-hizi wa Mashahidi wa Yehova.

      6. (a) Ni nini linalomaanishwa na “vitu vilivyopo”? (b) Kwa nini sisi tunaweza kuwa na uhakika kwamba hali katika kundi la Wakristo wapakwa-mafuta leo lazima ziwe zinafanana na zile za siku ya Yohana?

      6 Mwingi wa unabii katika Ufunuo ungetimizwa baada ya wakati wa Yohana. Ulirejezea “vitu ambavyo vitatukia baada ya hivi.” Lakini shauri kwa yale makundi saba linashughulika na “vitu vilivyopo,” hali ambazo zilikuwamo kweli kweli katika hayo makundi saba wakati ule. Jumbe hizo zilikuwa misaada yenye thamani kwa wazee waaminifu waliowekwa rasmi katika makundi hayo saba, vilevile makundi mengine yote ya Wakristo wapakwa-mafuta ya wakati huo.b Kwa kuwa ile njozi ina utumizi mkuu katika siku ya Bwana, yale anayosema Yesu yanatoa onyo kwamba hali kama hizo zingetarajiwa ziweko katika kundi la Wakristo wapakwa-mafuta la siku yetu wenyewe.—Ufunuo 1:10, 19.

  • Yohana Aona Yesu Aliyetukuzwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • b Katika karne ya kwanza, kundi lilipopokea barua kutoka kwa mtume, ilikuwa desturi kuzungusha barua hiyo kwa makundi mengine ili yote yaweze kunufaika na shauri.—Linga Wakolosai 4:16.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki