Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mtu Mzuri Hukubaliwa na Mungu’
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Januari 15
    • “Mizizi Isiyoweza Kung’olewa”

      Bila shaka, mtu mwema ni mwadilifu na hufuatia haki. Kwa hiyo sifa ya uadilifu ni muhimu ili kukubaliwa na Yehova. Mfalme Daudi aliimba hivi: “Maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.” (Zaburi 5:12) Akitofautisha hali ya mtu mwadilifu na mwovu, Sulemani asema: “Mtu hatathibitika kwa njia ya mwovu; shina la mwenye haki halitaondolewa kamwe.”—Mithali 12:3.

      Huenda waovu wakaonekana kana kwamba wamefanikiwa. Fikiria mfano wa mtunga-zaburi Asafu. Anasema: “Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka, hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza.” Kwa nini? Asafu anajibu: “Niliwaonea wivu wenye kujivuna, nilipoona hali ya amani ya wasio haki.” (Zaburi 73:2, 3) Lakini alipokaribia patakatifu pa hekalu la Mungu, alitambua kwamba Yehova amewaweka mahali penye utelezi. (Zaburi 73:17, 18) Mafanikio ambayo huenda waovu wakapata ni ya muda tu. Hivyo basi, mbona tuwaonee wivu?

      Kwa upande mwingine, mtu ambaye anakubaliwa na Mungu, yu imara. Akitumia mfano wa mti wenye mizizi imara, Sulemani anasema: “Watu wema wana mizizi isiyoweza kung’olewa.” (Mithali 12:3, The New English Bible) Mizizi isiyoonekana ya mti mkubwa sana kama ule uitwao sequoia ambao unapatikana huko California inaweza kusambaa kwa ekari kadhaa na kuwa ngome wakati wa mafuriko na pepo kali. Mti huo mkubwa hata unaweza kustahimili tetemeko kubwa la ardhi.

      Kama mizizi hiyo inayopenya kwenye udongo ulio na rutuba, akili na mioyo yetu inapaswa kupenya katika Neno la Mungu na kutwaa maji ya uhai. Kwa hiyo imani yetu inakuwa thabiti na yenye nguvu, nalo tumaini letu linakuwa hakika na imara. (Waebrania 6:19) ‘Hatutachukuliwa huku na huku na kila upepo wa fundisho lisilo la kweli.’ (Waefeso 4:14) Bila shaka, tutahisi matokeo ya majaribu makali na hata kuogopa wakati kunapotokea janga. Lakini ‘shina letu halitaondolewa.’

  • “Mtu Mzuri Hukubaliwa na Mungu’
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Januari 15
    • Mawazo Huongoza Kwenye Matendo, Kisha Matokeo

      Mawazo huongoza kwenye matendo, nayo matendo huongoza kwenye matokeo. Sulemani sasa anaonyesha jinsi mawazo huongoza kwenye matendo, akitofautisha wenye haki na waovu. Anasema: “Mawazo ya mwenye haki ni adili; bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa. Maneno ya waovu huotea damu; bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa.”—Mithali 12:5, 6.

      Mawazo ya watu wema ni ya uadilifu nayo huwaongoza kutenda kwa njia ya haki bila ubaguzi. Nia ya wenye haki ni njema kwa kuwa wao huchochewa na upendo wao kwa Mungu na wanadamu wenzao. Kwa upande mwingine, waovu huchochewa na ubinafsi. Kwa hiyo, mbinu zao—njia wanazotumia kutimiza malengo yao—ni za udanganyifu. Matendo yao ni yenye hila. Hawasiti kuwawekea mtego watu wasio na hatia, labda mahakamani, kwa kuwasilisha mashtaka bandia. Maneno yao “huotea damu” kwa sababu wanataka kuwadhuru watu wasio na hatia. Wenye haki huepuka hatari hiyo kwa sababu wanafahamu mbinu za waovu na wana hekima ambayo huwasaidia kuwa chonjo. Hata wanaweza kuwaonya watu wasio waangalifu na kuwaokoa kutokana na mbinu za waovu.

      Ni nini kitakachowapata wenye haki na waovu? “Waovu huangamia, hata hawako tena; bali nyumba ya mwenye haki itasimama,” ajibu Sulemani. (Mithali 12:7) Kichapo fulani cha kitaalamu kinasema kwamba nyumba “inamaanisha familia na kitu chochote chenye thamani cha mtu huyo, ambacho humwezesha kuishi.” Inaweza kumaanisha wazao wa mwenye haki. Vyovyote iwavyo, jambo linalotajwa na methali hiyo ni wazi: Mwenye haki atasimama imara wakati wa magumu.

  • “Mtu Mzuri Hukubaliwa na Mungu’
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Januari 15
    • Mwenye Haki Husitawi

      “Asiye haki hutamani nyavu za wabaya,” asema mfalme mwenye hekima. (Mithali 12:12a) Asiye haki hufanya hivyo jinsi gani? Hufanya hivyo kwa kutamani nyara iliyopatikana kwa njia isiyofaa.

      Tunaweza kusema nini kuhusu mtu mwema? Anapenda nidhamu na ana imani yenye nguvu. Ni mwadilifu, mwenye busara, mnyenyekevu, mwenye huruma na bidii. Na “shina lao wenye haki huleta matunda,” au “husitawi” asema Sulemani. (Mithali 12:12b) “Mzizi wa mwenye haki utadumu milele,” yasema tafsiri ya An American Translation. Mtu wa namna hiyo ni imara na salama. Kwa kweli ‘mtu mzuri atakubaliwa na BWANA.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki