-
Rumania2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Petre Ranca aliwekwa kuwa katibu wa ofisi ya Mashahidi wa Yehova nchini Rumania mwaka wa 1938. Kwa sababu ya wadhifa huo na kazi yake ya kutafsiri, alikuwa mmojawapo wa watu waliosakwa sana na maofisa wa Idara ya Usalama. Hatimaye alikamatwa mwaka wa 1948, na baada ya kuachiliwa na kukamatwa mara kadhaa akafikishwa mahakamani pamoja na Martin Magyarosi na Pamfil Albu mwaka wa 1950. Alishtakiwa kwa uwongo kuwa mwanachama wa kikundi cha wapelelezi cha Marekani, na alivumilia kifungo cha miaka 17 katika magereza mabaya zaidi nchini humo, yaani, Aiud, Gherla, na Jilava. Pia alizuiliwa nyumbani kwa miaka mitatu katika Mkoa wa Galaţi. Ndugu huyo mwaminifu, aliyekuwa na tumaini la kimbingu, alimtumikia Yehova kwa moyo wote hadi alipokufa mnamo Agosti 11, 1991.
-
-
Rumania2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 138]
Petre Ranca
-