-
Rumania2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
1938: Serikali yafunga kabisa ofisi ya tawi ya Rumania, huko Bucharest.
-
-
Rumania2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
1946: Watu wapatao 15,000 wahudhuria kusanyiko la kwanza nchini humo linalofanyiwa Bucharest.
-
-
Rumania2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
1995: Ofisi ya tawi ya Rumania yafunguliwa upya huko Bucharest.
-
-
Rumania2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Baadaye ndugu hao wawili walitumwa Bucharest, ambako waliwasaidia wengi kupata ujuzi sahihi wa Neno la Mungu. Mtu mmoja aliyethamini msaada huo aliandika hivi: “Ninamshukuru Mungu kwa kuwatuma Ndugu Emanoil na Onisim, ambao walijitahidi sana kunisadikisha na kunifundisha Neno la Mungu. Bwana atafanya kazi kubwa katika mji huu, lakini uvumilivu unahitajika.”
-
-
Rumania2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Daniel, ambaye ni mtu wa ukoo wa Ioan anasema hivi: “Ioan Rus aliitwa jeshini mwaka wa 1914. Kwa sababu alikataa kujiunga na jeshi alipelekwa Bucharest na kuhukumiwa kifo. Alilazimishwa kuchimba kaburi lake mwenyewe na kusimama kando yake huku akikabili kikosi cha wauaji. Ofisa mkuu alimruhusu Ioan kusema maneno yake ya mwisho. Ioan akaamua kutoa sala kwa sauti. Wanajeshi hao waliguswa sana na sala ya Ioan hivi kwamba walikataa kumuua. Ndipo, ofisa mkuu akampeleka mwanajeshi mmoja kando na kumwahidi likizo na mshahara wa miezi mitatu kwa kumpiga mfungwa huyo risasi. Mtu huyo alikubali, na akapata likizo kwa kumuua Ioan.”
-