Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Samweli wa Kwanza
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Machi 15
    • SAMWELI ACHUKUA NAFASI YA ELI AKIWA MWAMUZI

      (1 Samweli 1:1–7:17)

      Ni wakati wa Sherehe ya Kukusanya, naye Hana, ambaye anaishi Rama ana furaha nyingi.a Yehova amejibu sala zake, naye amezaa mwana. Ili kutimiza nadhiri yake, Hana anampeleka mwana wake Samweli akatumikie kwenye “nyumba ya Yehova.” Huko, mvulana huyo anakuwa “mhudumu wa Yehova mbele ya Eli kuhani.” (1 Samweli 1:24; 2:11) Samweli akiwa bado mchanga sana, Yehova anazungumza naye na kutoa hukumu dhidi ya nyumba ya Eli. Samweli anapozeeka, watu wote wa Israeli wanatambua kwamba yeye ni nabii wa Yehova.

      Mwishowe, Wafilisti wanashambulia Israeli. Wanalichukua Sanduku na kuwauwa wana wawili wa Eli. Anapopata habari hizo, Eli aliye mzee anakufa, akiwa “amehukumu Israeli kwa miaka 40.” (1 Samweli 4:18) Kuwa na Sanduku hilo kunatokeza msiba kwa Wafilisti, hivyo wanalirudisha kwa Waisraeli. Sasa Samweli anakuwa mwamuzi wa Israeli, na kuna amani katika nchi.

  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Samweli wa Kwanza
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Machi 15
    • MFALME WA KWANZA WA ISRAELI —JE, ALIFANIKIWA AU HAKUFANIKIWA?

      (1 Samweli 8:1–15:35)

      Samweli ni mwaminifu kwa Yehova maisha yake yote, lakini wanawe hawatembei katika njia za Mungu. Wanaume wa Israeli wanapoomba mfalme wa kibinadamu, Yehova anakubali ombi lao. Samweli anafuata mwongozo wa Yehova naye anamtia mafuta Sauli, Mbenyamini mwenye sura nzuri, awe mfalme. Sauli anaimarisha cheo chake akiwa mfalme kwa kuwashinda Waamoni.

      Yonathani, mwana wa Sauli aliye shujaa anashinda kikosi cha askari Wafilisti. Jeshi kubwa la Wafilisti linashambulia Israeli. Sauli anaogopa sana na kwa kutotii, yeye mwenyewe anatoa dhabihu ya kuteketezwa. Akiwa tu na mchukua-silaha wake, Yonathani mwenye ujasiri anashambulia kituo kingine cha Wafilisti. Hata hivyo, Sauli anaapa bila kufikiri, na hivyo ushindi huo unakosa kukamilika. Sauli anaanza “kupiga vita kuzunguka pande zote” juu ya adui zake wote. (1 Samweli 14:47) Ingawa anawashinda Waamaleki, Sauli anakosa kumtii Yehova na kuhifadhi kile ‘kilichotengwa kwa ajili ya kuharibiwa.’ (Mambo ya Walawi 27:28, 29) Kwa sababu hiyo, Yehova anamkataa Sauli kuwa mfalme.

  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Samweli wa Kwanza
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Machi 15
    • KIJANA MCHUNGAJI ACHAGULIWA KUWA MFALME

      (1 Samweli 16:1–31:13)

      Samweli anamtia mafuta Daudi wa kabila la Yuda ili awe mfalme wakati ujao. Muda mfupi baadaye, Daudi anamuua Goliathi, jitu la Wafilisti kwa jiwe la kombeo. Urafiki wa karibu unakua kati ya Daudi na Yonathani. Sauli anamweka Daudi kuwa mkuu wa mashujaa wake wa vita. Ili kushangilia ushindi mwingi wa Daudi, wanawake wa Israeli wanaimba hivi: “Sauli amepiga maelfu yake, na Daudi makumi ya maelfu yake.” (1 Samweli 18:7) Akiwa amejawa na wivu, Sauli anajaribu kumuua Daudi. Baada ya kushambuliwa mara tatu na Sauli, Daudi anatoroka na kuwa mkimbizi.

      Katika miaka yake akiwa mkimbizi, Daudi anahifadhi uhai wa Sauli mara mbili. Pia anakutana na Abigaili mrembo na mwishowe anamwoa. Wafilisti wanaposhambulia Israeli, Sauli anamtafuta Yehova. Lakini Yehova amemwacha. Tayari Samweli amekufa. Akiwa na wasiwasi mwingi, Sauli anamwendea mwanamke mwenye kuwasiliana na pepo, naye anamwambia kwamba atauawa vitani na Wafilisti. Wakati wa mapigano hayo, Sauli anajeruhiwa vibaya, nao wana wake wanauawa. Simulizi hilo linamalizia kwa kuonyesha Sauli akifa bila kufanikiwa. Bado Daudi yuko mafichoni.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki