-
Nguvu za Kuumba—“Aliyezifanya Mbingu na Nchi”Mkaribie Yehova
-
-
6. Biblia inaonyeshaje kwamba idadi ya nyota ni kubwa sana wanadamu wasiweze kuhesabu?
6 Lakini idadi ya nyota inastaajabisha zaidi ya ukubwa wake. Kwa kweli, Biblia inasema kwamba nyota haziwezi kuhesabiwa, kama vile “mchanga wa bahari” usivyoweza kuhesabiwa. (Yeremia 33:22) Maneno hayo yanadokeza kwamba kuna nyota nyingi sana ambazo hatuwezi kuona pasipo vifaa maalumu. Endapo mwandikaji wa Biblia, kama Yeremia, angetazama angani wakati wa usiku na kujaribu kuhesabu nyota zionekanazo, angefaulu kuhesabu nyota zipatazo 3,000 hivi. Wanadamu huweza kuona idadi hiyo tu ya nyota katika anga jangavu la usiku bila kutumia vifaa maalumu. Idadi hiyo yaweza kulinganishwa na idadi ya chembe za mchanga zinazoweza kujaza kiganja kimoja tu cha mkono. Hata hivyo, idadi halisi ya nyota haijulikani, ni nyingi kama mchanga wa bahari. Ni nani awezaye kuhesabu idadi kubwa hivyo?b
-
-
Nguvu za Kuumba—“Aliyezifanya Mbingu na Nchi”Mkaribie Yehova
-
-
b Watu fulani hufikiri kwamba watu walioishi katika nyakati za Biblia walitumia darubini fulani ya kienyeji. Wanatoa sababu kwamba watu walioishi nyakati hizo hawangeweza kujua kwamba idadi ya nyota ni kubwa sana wanadamu wasiweze kuhesabu. Makisio hayo yasiyo na msingi hayamheshimu wala kumtambua Yehova, Mtungaji wa Biblia.—2 Timotheo 3:16.
-