Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maajabu na Mafumbo Katika Bahari
    Amkeni!—2000 | Novemba 22
    • Kusudi la safari ya chombo cha Alvin lilikuwa kutafuta chemchemi za maji moto—chemchemi zilizo chini ya bahari zinazomimina michirizi ya maji moto baharini.

  • Maajabu na Mafumbo Katika Bahari
    Amkeni!—2000 | Novemba 22
    • Taa zao zilimulika matundu kadhaa yenye maji moto yanayomeremeta kwenye sakafu ya bahari, ambako kwa kawaida maji hukaribia kuwa barafu. Karibu na matundu hayo, jambo lenye kustaajabisha hata zaidi lilitokea—jamii nzimanzima za viumbe ambao hawakuwa wamejulikana awali waliibuka. Miaka miwili baadaye, watafiti waliokuwa katika Alvin waligundua matundu yenye maji moto kupindukia yanayoitwa smokers katika Safu ya Milima ya Pasifiki Mashariki karibu na pwani ya Mexico. Baadhi ya matundu hayo hufanyiza mabomba ya ajabu, mengine hufikia kimo cha meta sita.

  • Sakafu ya Bahari—Siri Zake Zafunuliwa
    Amkeni!—2000 | Novemba 22
    • Kwa sababu ya hali yake ya kubadilika-badilika na milipuko ya volkano, safu ya milima ya katikati ya bahari ina vijito tele vya volkano na matundu mengi ya maji moto. Mchanganyiko moto sana wenye sumu wa maji na madini ya ardhini hububujika kutoka kwenye matundu hayo. Lakini, jambo la kushangaza ni kwamba mazingira hayo yasiyokalika, yanayokumbwa na kanieneo zinazozidi kwa mbali sana zile zilizo katika usawa wa bahari, huvutia viumbe chungu nzima—badala ya kuvifukuza!

  • Sakafu ya Bahari—Siri Zake Zafunuliwa
    Amkeni!—2000 | Novemba 22
    • Uvundo huo hausababishwi na kuoza, bali na hidrojeni salfaidi—kemikali yenye sumu kali inayotoa uvundo wenye kuchukiza ambayo imejaa kote katika matundu ya maji moto. Maji yanayotoka katika matundu hayo yana asidi kali na metali nyingi, kutia ndani shaba, magnesi, chuma, na zinki. Badala tu ya kustahimili katika mazingira hayo—ambayo yamelinganishwa na mahali pa kutupa takataka zenye sumu—tube worm na viumbe wengine husitawi humo!

  • Sakafu ya Bahari—Siri Zake Zafunuliwa
    Amkeni!—2000 | Novemba 22
    • Nishati Kutoka Katika Kiini cha Dunia

      Kwa akili nyingi, Muumba ameandaa nishati inayohitajiwa kutoka kwa kiini cha dunia kupitia kwa matundu ya maji moto na ile kemikali yenye uvundo ya hidrojeni salfaidi. Hidrojeni salfaidi ambayo ni “nuru ya jua” ya jamii zinazoishi katika matundu ya baharini, huandaa nishati inayohitajiwa na bakteria katika utengenezaji wa chakula.

  • Sakafu ya Bahari—Siri Zake Zafunuliwa
    Amkeni!—2000 | Novemba 22
    • Nuru ya Ajabu!

      Mnamo mwaka wa 1985, wanasayansi walishangaa kuona uduvi wenye sehemu mbili zinazoshabihi macho wakiwa karibu na matundu ya baharini, sehemu hizo zisizo na lenzi zina kemikali zinazotambua nuru kwa wepesi. Bila shaka, swali walilofikiria kwanza ni, Wanyama hao wanaweza kuona nini katika giza totoro? Ili kupata jawabu, watafiti walitumia kamera ya tarakimu yenye nguvu sana, kama ile inayotumiwa kupiga picha nyota hafifu sana. Waliielekeza kamera hiyo penye tundu, wakazima taa zote, kisha wakapiga picha.

      Matokeo yalishangaza. Picha kwenye kompyuta ilifunua “nuru maridadi, dhahiri na yenye kung’aa” ukingoni mwa bomba yalimotokea maji moto, asema mwanasayansi Cindy Lee Van Dover. Je, uduvi hutumia nuru hii ya ajabu, isiyoweza kuonwa kwa macho ya mwanadamu? Vyovyote iwavyo, ugunduzi wa kwamba matundu ya maji moto hutoa nuru “waanzisha fani mpya kabisa ya utafiti,” aongezea Van Dover.

  • Sakafu ya Bahari—Siri Zake Zafunuliwa
    Amkeni!—2000 | Novemba 22
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 7]

      Matundu ya Maji Moto Ni Nini?

      Katika safu ya milima ya volkano iliyo katikati ya bahari, maji ya bahari hupenya nyufa zilizo katika tabaka la juu la dunia na kuingia katika maeneo yenye joto kali kupindukia. Maji hayo huchemka kabisa, kisha hufyonza kemikali kadhaa yanapopenya miamba. Pia husukasuka, na kufika kwenye sakafu ya bahari, na hivyo hufanyiza matundu ya maji moto—chemchemi za maji moto. Chemchemi hizo “bila shaka zina nguvu na huvutia sana kama chemchemi zilizo ardhini,” chasema kichapo kimoja.

      Isitoshe, joto la chemchemi hizo zilizo kwenye sakafu ya bahari laweza kufikia nyuzi Selsiasi 400, moto zaidi kushinda risasi iliyoyeyuka! Lakini kwa sababu ya kanieneo ya bahari iliyo juu, kioevu hicho chenye joto sana hakiwi mvuke. Jambo la kushangaza ni kwamba milimeta chache tu kutoka kwa mkondo wa maji moto, kwa kawaida joto la wastani la bahari huwa nyuzi Selsiasi moja au mbili tu kushinda barafu. Madini yanayotoka kwa maji hayo moto yanayopoa upesi hujikusanya kwenye sakafu ya bahari, ambapo yanafanyiza vilima na mabomba. Mabomba hayo yaweza kuwa na kimo cha meta tisa. Kwa kweli, bomba moja lenye kimo cha meta 45 na kipenyo cha meta 10 hivi liligunduliwa, na bado lilikuwa likirefuka!

      Matundu ya maji moto yanaweza kububujika na kutulia ghafula, na hilo ni hatari sana kwa viumbe wanaoishi karibu na matundu hayo. Hata hivyo, viumbe fulani huepuka hatari kwa kuhamia kwenye matundu mengine.

      [Hisani]

      P. Rona/OAR/National Undersea Research Program

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki