-
Maajabu na Mafumbo Katika BahariAmkeni!—2000 | Novemba 22
-
-
Bonde la Ufa la Galápagos lilifaa kwa sababu ni sehemu ya bonde lililo baharini lenye utendaji mkubwa wa volkano, ambalo limezingirwa na safu tata ya milima inayozunguka ulimwenguni pote, inayoitwa safu ya milima iliyo katikati ya bahari. Safu hiyo ndefu ajabu yenye urefu wa mlalo wa zaidi ya kilometa 65,000, hujipinda-pinda na kuzunguka dunia yote kama mshono ulio kwenye mpira wa tenisi. Kama haingefunikwa na bahari, “mara moja [ingekuwa] sehemu kubwa zaidi katika uso wa dunia, ikisambaa kwenye eneo linalozidi eneo linalofunikwa na safu zote kubwa za milima duniani,” aandika Jon Erickson katika kitabu chake kiitwacho Marine Geology.
Sehemu yenye kutokeza hasa ya safu ya milima iliyo katikati ya bahari ni kwamba kwa kweli ni safu mbili—safu mbili za milima zilizo sambamba na zenye kimo cha meta 3,000 kutoka kwenye sakafu ya bahari. Kati ya safu hizo kuna nyufa kubwa zaidi duniani—makorongo yenye upana wa kilometa zipatazo 20 na kina cha kilometa 6—zenye kina ambacho ni mara nne zaidi ya kina cha lile Korongo Kuu la Amerika Kaskazini! Milipuko mikali ya volkano hutukia chini ya nyufa hizo zilizo bondeni. Wanasayansi walipochunguza kwa mara ya kwanza sehemu ya safu hiyo ya milima kwenye Bahari ya Atlantiki, inayoitwa Safu ya Milima Iliyo Katikati ya Atlantiki, vifaa vyao vilifunua milipuko mikali ya volkano “hata ilionekana ni kana kwamba sehemu ya ndani ya Dunia ilikuwa ikitoka nje,” asema Erickson.
-
-
Sakafu ya Bahari—Siri Zake ZafunuliwaAmkeni!—2000 | Novemba 22
-
-
Miamba hiyo husogea-sogea. Mahali inapotengana, inaacha pengo na kutokeza nyufa katika safu ya milima ya katikati ya bahari. Ulimwenguni pote, miamba hiyo husogea kwa mwendo wa wastani wa sentimeta tatu hivi kwa mwaka.
Kulingana na nadharia ya miamba ya dunia, kadiri miamba inavyotengana karibu na safu ya milima ya katikati ya bahari, ndivyo inavyoruhusu miamba moto iliyo katika tabaka la katikati la dunia, chini tu ya tabaka la juu, ipande. Myeyuko huo moto hufanyiza tabaka jipya baharini katikati ya miamba mikuu miwili, lakini miamba hiyo haiungani. Badala yake, inasukumwa mbali zaidi, na hilo hufanya safu ya milima ishabihi kidonda kikubwa kisichopona.
-