-
Kwa Nini Maneno Yako Ni MuhimuAmkeni!—2011 | Juni
-
-
Maoni ya Biblia
Kwa Nini Maneno Yako Ni Muhimu
Baada ya kuzungumza na mwanamke fulani mzee kwa heshima, na bila kujua kwamba mikrofoni haikuwa imezimwa, waziri mkuu anasema kwamba mwanamke huyo anashikilia sana maoni yake bila kutumia akili, kisha analalamika kwamba wafanyakazi wake walipaswa kumzuia. Maneno hayo ya kumchambua mwanamke huyo yanalishtua taifa zima. Jina lake likiwa limechafuka, waziri huyo mkuu anapoteza kiti chake siku nane tu baadaye katika uchaguzi uliofuata.
HAKUNA mwanadamu anayeweza kuuzuia ulimi wake kikamili. (Yakobo 3:2) Lakini, kisa kilichotajwa hapo juu kinaonyesha kwamba maneno yako ni muhimu. Jina lako, kazi yako, na hata mahusiano yako na watu wengine yanategemea maneno unayosema na jinsi unavyoyasema.
Lakini je, ulijua kwamba maneno yako ni muhimu kwa sababu nyingine? Biblia inaeleza kwamba maneno yako huonyesha jinsi ulivyo kwa ndani, utu wako. Yesu alisema: “Kinywa kinasema kutokana na mambo yaliyojaa katika moyo.” (Mathayo 12:34) Kwa kuwa maneno yako huonyesha jinsi unavyohisi na kufikiri, ni muhimu uchunguze usemi wako kwa undani zaidi.
-
-
Kwa Nini Maneno Yako Ni MuhimuAmkeni!—2011 | Juni
-
-
Fikiri kabla ya kusema. “Kuna mtu anayesema bila kufikiri kama kwa upanga unaochoma, lakini ulimi wa mwenye hekima huponya,” inasema Methali 12:18. Ikiwa mara nyingi wewe ‘huchoma,’ au kuumiza hisia za wengine, ni vizuri kujitahidi kufikiri kabla ya kusema. Fuata shauri hili zuri linalopatikana kwenye Methali 15:28: “Moyo wa mwadilifu hutafakari ili kujibu, lakini kinywa cha waovu hububujika mambo mabaya.”
Jaribu kuweka mradi. Mwezi wote ujao, azimia kutosema jambo la kwanza linalokuja akilini mwako, hasa unapochokozwa. Badala yake, fikiria maandiko ambayo yametajwa katika habari hii, na ujitahidi sana kuzungumza kwa hekima, upendo, na utulivu. (Methali 15:1-4, 23)
-