-
Historia ya Saa za MkononiAmkeni!—2005 | Mei 22
-
-
Uchague Saa Gani?
Bila shaka, ungependa kuwa na saa inayovutia. Kwa watu wengi hiyo inamaanisha kuwa na saa nzuri, inayofanya kazi, na yenye sura ya kupendeza. Isitoshe, Michael anapendekeza ufikirie kwa makini mambo yatakayoipata saa yako. Je, utaivaa kila siku au katika pindi za pekee tu? Je, itahimili kugongwa-gongwa au viwango tofauti vya joto? Kwa mfano, kemikali au maji ya chumvi yanaweza kuharibu mikanda na vifuniko fulani vya saa. Kwa hiyo ni jambo la hekima kufikiria mambo hayo.
Kuhusu bei, unapaswa kuwa na bajeti na kuifuata. Kwa kawaida, saa za majira ni ghali kuliko saa za betri. Hata hivyo, kumbuka kwamba utendaji uleule hutumika katika saa nyingi. Kwa kawaida, sehemu ya nje na ile sehemu ambayo huonyesha wakati huwa zimebuniwa na kuundwa vizuri. Mara nyingi, bei hutofautiana tu kwa sababu ya sehemu zisizofanya kazi kama vile kifuniko na mkanda. Kwa hiyo, ikiwa saa ni ya bei ghali haimaanishi kwamba ni sahihi zaidi au ni yenye kutegemeka.—Ona sanduku lililo juu.
-
-
Historia ya Saa za MkononiAmkeni!—2005 | Mei 22
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 24]
Ni Saa Gani Inayokufaa Zaidi?
AINA: Kronografu ina vifaa fulani vya kuhesabia vipindi vifupi vya wakati, nacho ni chombo kinachofaa ikiwa unataka kurekodi matukio. Saa isiyopenya maji inafaa katika michezo. Ikiwa wewe husahau kuongeza majira, kumbuka kwamba saa ya betri haihitaji kuongezwa majira. Pia huhitaji kutia majira saa zinazojitia majira, ambazo huongezwa majira mvaaji anapotikisa mkono wake.
USAHIHI: Ikiwa unathamini sana saa sahihi, huenda ukafikiria kununua kronometa, saa inayopima wakati kwa usahihi na kutimiza viwango rasmi vinavyokubalika kimataifa. Jinsi saa za betri zilivyoundwa huzifanya ziwe sahihi zaidi. Saa ya kisasa ya majira inayopiga mara 28,800 kwa saa hutikisika mara nne kwa sekunde. Linganisha saa hiyo na saa ya betri ambayo hutikisika kati ya mara 10,000 na 100,000 kwa sekunde!
KUONYESHA WAKATI: Kuna saa ambayo huonyesha wakati kwa kutumia tarakimu. Nyingine hutumia mishale inayozunguka uso wa saa. Saa za tarakimu zinaweza kupiga kengele, kuonyesha tarehe, kanda fulani ya wakati, na vipindi vya muda vinavyopita. Saa zenye mishale huonyesha wakati katika njia rahisi na yenye kueleweka, kwa kutupia tu jicho mishale yake.
UTUNZAJI: Tofauti na saa ya betri, kwa kuwa saa ya majira huendeshwa kwa springi yenye nguvu, inaweza kuacha kufanya kazi kwa urahisi kwa sababu ya uchafu au vumbi. Hata hivyo, saa yako ya majira inahitaji utunzaji zaidi kuliko saa ya betri, ili iendelee kufanya kazi bila matatizo. Kwa kuwa saa za betri hazina sehemu zozote zinazosonga, hazihitaji utunzaji wowote isipokuwa tu kubadili betri.
-