Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Jina Jipya”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu.” (Isaya 62:10) Katika kisa cha kwanza, inaelekea kuwa mwito huu unamaanisha kupita na kutoka nje ya malango ya jiji ya Babilonia ili kurudi Yerusalemu. Hao wenye kurudi wanapaswa kuondoa mawe njiani ili kurahisisha safari na kuinua ishara ya kuonyesha njia ya kupitia.—Isaya 11:12.

  • “Jina Jipya”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 21, 22. Yehova amesimamisha ishara gani ili iwaongoze wale wanaotoka katika dini ya uwongo, nasi tunajuaje?

      21 Mwaka wa 537 K.W.K., jiji la Yerusalemu likawa ishara iliyowavutia mabaki Wayahudi ili warudi wakajenge hekalu upya. (Isaya 49:22) Mwaka wa 1919, mabaki watiwa-mafuta walipokombolewa kutoka kwenye utumwa wa dini ya uwongo, hawakutanga-tanga ovyo-ovyo. Walijua pa kwenda, kwa maana Yehova alikuwa amesimamisha ishara kwa ajili yao. Ishara gani? Ishara ile ile iliyotabiriwa kwenye Isaya 11:10, inayosema hivi: ‘Itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese litasimama kuwa ishara kwa kabila za watu.’ Mtume Paulo anatumia maneno hayo kumhusu Yesu. (Waroma 15:8, 12) Ndiyo, ile ishara ni Kristo Yesu, anayetawala akiwa Mfalme juu ya Mlima Sayuni wa kimbingu!—Waebrania 12:22; Ufunuo 14:1.

      22 Wakristo watiwa-mafuta na kondoo wengine pia wamekusanyika kumzunguka Yesu Kristo ili wajihusishe katika ibada ya Mungu Aliye Juu Zaidi inayounganisha watu. Utawala wake unasaidia kutetea enzi kuu ya Yehova ya ulimwengu mzima na kubariki watu wa mataifa yote ya dunia ambao ni wanyofu moyoni. Je, hiyo si sababu ya kumfanya kila mmoja wetu ajiunge katika kumtukuza kwa kumpa sifa?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki