Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Furahia Dunia Yetu Maridadi
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Februari 15
    • Na kama wanafunzi wanavyojifunza shuleni, mfumo mzima wa jua unazunguka katikati ya kikundi chetu cha nyota kinachoitwa Kilimia. Lakini katika kikundi chetu cha nyota, jua ni moja tu kati ya nyota zaidi ya bilioni 100 zinazozunguka pamoja.

      Nguvu za uvutano zinashikilia kikundi chetu cha nyota pamoja na vikundi vingine 35 hivi vya nyota. Makundi makubwa zaidi ya nyota yana maelfu ya vikundi vya nyota. Inaelekea kwamba mfumo wetu wa jua haungekuwa imara sana ikiwa ungekuwa katika kundi kubwa zaidi lenye vikundi vingi sana vya nyota. Lakini, kama ilivyo, ni maeneo machache katika ulimwengu mzima “yanayofaa kwa ajili ya uhai tata kama wetu,” wanasema Guillermo Gonzalez na Jay W. Richards katika kitabu chao (The Privileged Planet).

  • Mfumo Wetu wa Pekee wa Jua—Jinsi Ulivyotokea
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Februari 15
    • Mfumo Wetu wa Pekee wa Jua—Jinsi Ulivyotokea

      KUNA mambo mengi yanayofanya mfumo wetu wa jua uwe wa pekee katika ulimwengu mzima. Mfumo wetu wa jua uko kati ya mikono miwili inayozunguka ya kikundi chetu cha Kilimia katika eneo ambalo halina nyota nyingi sana likilinganishwa na maeneo mengine. Karibu nyota zote tunazoweza kuona usiku ziko mbali sana hivi kwamba zinapotazamwa kwa darubini kubwa zaidi, zinaonekana kama madoa madogo ya nuru. Je, mfumo wetu wa jua ulipaswa kuwa mahali ulipo?

      Ikiwa mfumo wetu wa jua ungekuwa karibu na sehemu ya katikati ya Kilimia, tungepata madhara kwa sababu ya kuwa katika eneo lenye msongamano mkubwa wa nyota. Kwa mfano, inaelekea kwamba mzunguko wa dunia ungevurugwa na hilo lingeathiri sana uhai wa wanadamu. Kama ilivyo, inaonekana kwamba mfumo wa jua upo mahali panapofaa kabisa katika kikundi chetu cha nyota ili kuepuka hatari hizo na nyinginezo. Hatari hizo zinatia ndani kuongezeka kwa joto mfumo wetu unapopita katika mawingu ya gesi na miale hatari inayotokana na nyota zinazolipuka.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki