Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Viwango Vyabadilika na Matumaini Yavunjwa
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Juni 1
    • Familia na Viwango vya Maadili

      Namna gani mabadiliko katika viwango vya familia na maadili? Matokeo ya mabadiliko hayo yanaweza kuwa yenye madhara makubwa sana. Ripoti za hivi karibuni kuhusu kuvunjika kwa familia, kufanya ngono ovyoovyo, na kudhulumiwa kwa watoto, ambako kumeenea sana, huchukiza wengi na huthibitisha kwamba tunaishi wakati ambapo viwango vinazidi kushuka. Familia za mzazi mmoja, watoto wanaolelewa na “wazazi” wa jinsia moja, na hali ya kuogofya ya kunajisiwa kwa watoto wanaotunzwa na halmashauri za mitaa, ni mambo yanayofanywa na watu wanaokataa viwango vinavyokubalika. Watu wengi wanakuwa “wenye kujipenda wenyewe, . . . wasio na shauku ya kiasili, . . . wasio na upendo wa wema, . . . wenye kuzipenda raha badala ya kuwa wapenda Mungu,” kama vile Biblia ilivyotabiri miaka elfu mbili hivi iliyopita.—2 Timotheo 3:1-4.

      Kushuka kwa viwango vya maadili huenda sambamba na kuvunja matumaini ya wengine bila kujali. Hivi majuzi, ukiukaji ulio wazi wa viwango vya juu vya kazi ya udaktari ulifunuliwa huko Hyde, mji ulio kaskazini mwa Uingereza, ambako wakazi waliwatumaini madaktari “walioheshimika na kutumainika.” Lakini inasikitisha kwamba alivunja matumaini yao. Jinsi gani? Ripoti za uchunguzi wa mahakama zilionyesha kwamba daktari mmoja alisababisha vifo vya angalau wanawake 15 aliokuwa anawatibu. Ilibidi polisi wachunguze upya vifo vya watu wengine 130 ambavyo vilisababishwa na daktari huyo. Daktari huyo alipatikana na hatia na kufungwa gerezani, jambo lililodhihirisha kadiri alivyokuwa amevunja matumaini ya wengine. Maofisa wawili wa gereza ambao huenda mama yao aliuawa na daktari huyo walipewa kazi nyingine ili wasilazimike kumtunza mfungwa huyo mwenye sifa mbaya. Si ajabu kwamba ripoti ya kesi hiyo kwenye gazeti la The Daily Telegraph ilimwita “Daktari ‘Ibilisi.’”

  • Unaweza Kutumaini Viwango vya Nani?
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Juni 1
    • Kwa Nini Viwango Vinashuka Leo?

      Biblia inaonyesha sababu inayofanya viwango vishuke leo. Ufunuo, kitabu cha mwisho cha Biblia, kinaeleza juu ya vita iliyopiganwa mbinguni, ambayo matokeo yake yameathiri wanadamu wote hadi leo. Mtume Yohana aliandika: “Vita ikatokea ghafula mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na joka kubwa, hilo joka na malaika zalo walipigana lakini halikuweza, wala mahali hapakupatikana mbinguni kwa ajili yao tena. Kwa hiyo likavurumishwa chini hilo joka kubwa mno, nyoka wa awali, yeye aitwaye Ibilisi na Shetani, anayeiongoza vibaya dunia nzima inayokaliwa; akavurumishwa chini kwenye dunia, na malaika zake wakavurumishwa chini pamoja naye.”—Ufunuo 12:7-9.

      Matokeo ya papo hapo ya vita hiyo yalikuwa nini? Yohana aliendelea kusema: “Kwa ajili ya hili teremeni, nyinyi mbingu nanyi mkaao ndani yazo! Ole wa dunia na wa bahari, kwa sababu Ibilisi ameteremka kwenu, akiwa na hasira kubwa, akijua ana kipindi kifupi cha wakati.”—Ufunuo 12:12.

      ‘Dunia ilipatwa na ole’ wakati Vita ya Kwanza ya Ulimwengu ilipoanza mwaka wa 1914 na kukomesha viwango vya wakati huo ambavyo vilikuwa tofauti sana na vya leo. “Vita Kuu ya 1914-1918 ni kama mpaka unaotenganisha wakati huo na wetu,” asema mwanahistoria Barbara Tuchman. ‘Vita hiyo Kuu ilisababisha vifo vya watu wengi ambao wangetimiza mambo yenye manufaa katika miaka iliyofuata. Iliharibu imani, ikabadili mawazo, na kusababisha madhara ya kudumu ya kukatisha tamaa, hivyo ikafanya kufikiri na mitazamo ya watu iwe tofauti na ilivyokuwa kabla ya vita hiyo.’ Mwanahistoria mwingine, Eric Hobsbawm, ana maoni kama hayo: ‘Tangu mwaka wa 1914, inasikitisha kwamba viwango ambavyo wakati huo vilionekana kuwa vya kawaida katika nchi zilizositawi vimeshuka sana kufikia hali ambayo mababu wetu wa karne ya 19 wangeviita viwango visivyo vya ustaarabu.’

      Katika kitabu chake Humanity—A Moral History of the Twentieth Century, mwandishi Jonathan Glover asema: “Jambo moja linalotambulisha wakati wetu ni kuzorota kwa sheria ya maadili.” Japo anatilia shaka sheria za maadili kwa sababu ya kuzorota kwa dini katika nchi za Magharibi, yeye anatoa tahadhari hii: “Wale miongoni mwetu ambao hawana imani na sheria ya maadili ya kidini, bado wanapaswa kutiwa wasiwasi kwa kuzorota kwake.”

      Leo, kuvunjwa kwa matumaini na matokeo yake mabaya—iwe ni katika biashara, siasa, au dini au hata katika mahusiano ya kibinafsi na ya familia—ni mojawapo ya mbinu mbovu za Shetani za kuwaletea wakaaji wa dunia ole. Shetani ameazimia kupigana vita hadi mwisho na kujaribu kuona kwamba wale wanaojitahidi kuishi kupatana na viwango vya Mungu wanaharibiwa pamoja naye.—Ufunuo 12:17.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki