Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nyota Zinafunua Nguvu za Mungu
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Mei 1
    • Jinsi Mungu Anavyotumia Nguvu Zake

      Yehova Mungu anatumia nguvu zake kuwategemeza wale wanaofanya mapenzi yake. Kwa mfano, mtume Paulo alitumia nguvu zake ili kuwafundisha wengine kumhusu Mungu. Paulo hakuwa malaika, lakini alitimiza kazi nyingi nzuri ingawa alikabili upinzani mkali. Jinsi gani? Alikiri kwamba alipokea “nguvu zinazopita zile za kawaida” kutoka kwa Mungu.—2 Wakorintho 4:7-9.

      Pia, Yehova Mungu ametumia nguvu zake kuwaharibu wale wanaovunja kimakusudi viwango vyake vya maadili. Yesu Kristo alizungumza kuhusu uharibifu wa Sodoma na Gomora na Gharika ya siku za Noa kuwa mifano ya jinsi Yehova anavyotumia nguvu zake ili kuwaharibu waovu tu. Yesu alitabiri kwamba hivi karibuni Yehova atatumia tena nguvu zake kuwaharibu wale wanaopuuza viwango Vyake.—Mathayo 24:3, 37-39; Luka 17:26-30.

  • Nyota Zinafunua Nguvu za Mungu
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Mei 1
    • Yehova alimwongoza nabii Isaya kuandika maneno haya yenye kufariji: “Yeye [Mungu] anampa nguvu mtu aliyechoka; naye huzijaza nguvu kamili kwa mtu asiye na nguvu zenye msukumo. Wavulana watachoka na pia kuzimia, na vijana hakika watajikwaa, lakini wale wanaomtumaini Yehova watapata nguvu mpya. Wataruka juu kwa mabawa kama tai. Watakimbia wala hawatazimia; watatembea wala hawatachoka.”—Isaya 40:29-31.

      Ikiwa unatamani kufanya mapenzi ya Mungu, unaweza kuwa na hakika kwamba atakupa roho yake takatifu ili ikutegemeze. Lakini unapaswa kumwomba Mungu akupe roho hiyo. (Luka 11:13) Kwa msaada wa Mungu, unaweza kuvumilia jaribu lolote na kupata nguvu za kutenda mambo yaliyo sawa.—Wafilipi 4:13.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki