-
Ala za Muziki Katika Israeli la KaleAmkeni!—2011 | Machi
-
-
Vinubi na Vinanda
Ala inayoitwa kinnor au “kinubi,” ilitumiwa sana katika Israeli la kale. Daudi aliicheza ili kumtuliza Mfalme Sauli. (1 Samweli 16:16, 23) Wasomi wana picha 30 hivi za vinubi vilivyochorwa kwenye kuta za mawe, sarafu, picha zilizotiwa nakshi, mabamba, na mihuri. Muundo wa ala hiyo ulibadilika kadiri karne zilivyopita. Mchezaji aliishika mikononi na kudonoa nyuzi zake kwa kutumia vidole au kwa kifaa fulani maalumu.
Ala inayoitwa nebel pia ilifanana na kinubi. Haijulikani kabisa nebel ilikuwa na nyuzi ngapi, ilikuwa kubwa kadiri gani, na ikiwa ilichezwa kwa kudonoa nyuzi zake au kwa kuzipiga. Hata hivyo, wasomi wengi wanadai kwamba mwanamuziki angeweza kuwa na nebel na vilevile kinubi.
-
-
Ala za Muziki Katika Israeli la KaleAmkeni!—2011 | Machi
-
-
[Picha katika ukurasa wa 16]
Sarafu ya karne ya pili W.K. iliyochorwa kinanda
-