Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jinsi Wainka Walivyopoteza Milki Yao Yenye Fahari
    Amkeni!—1998 | Januari 8
    • Macheo. Milima ya Andes yenye theluji kileleni ilikuwa imetiwa rangi nyororo ya nyekundu-nyeupe na miale ya nuru ichomozayo katika anga ya asubuhi. Wenye kuamka mapema miongoni mwa Wahindi hao walifurahia joto lenye kuondoa ubaridi wa usiku kwenye kimo cha meta 4,300. Polepole, miale ya jua ilifika chini na kuangaza hekalu la jua lililo katikati ya jiji kuu la Milki ya Inka, Cuzco (limaanishalo “Kitovu cha Ulimwengu”). Kuta zenye dhahabu ziliangaza miale ya jua. Michongo ya dhahabu tupu ya Ilama, vicuñas, na tai iling’aa katika bustani ya Wainkaa iliyokuwa mbele ya hekalu. Wapita-njia walipiga busu hewani katika kuabudu mungu wao, jua. Walishukuru kama nini kuwa hai na kubarikiwa na jua lililowapa riziki, kama walivyoamini!

  • Jinsi Wainka Walivyopoteza Milki Yao Yenye Fahari
    Amkeni!—1998 | Januari 8
    • Hekalu Lenye Kung’aa la Jua

      Katika jiji la kifalme la Cuzco, Wainka walipanga ukuhani kwa ajili ya kuabudu jua katika hekalu la mawe lililong’arishwa. Kuta za ndani zilipambwa kwa dhahabu safi na fedha. Pamoja na ukuhani, makao ya kipekee ya watawa yalianzishwa, kama lile lililojengwa upya katika hekalu la jua la Pachácamac, nje tu ya Lima. Mabikira warembo sana walizoezwa kutokea umri mchanga wa miaka minane kuwa ‘mabikira wa jua.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki