-
Linda Ngozi Yako!Amkeni!—2005 | Juni 8
-
-
Kansa inayoathiri chembe za ndani za ngozi ambayo hupata asilimia 5 tu ya watu wanaougua kansa ya ngozi, pia huanza katika sehemu ya juu ya ngozi. Inaonekana kwamba mojawapo ya visababishi vikuu vya aina hii ya kansa ni kujianika juani kwa vipindi virefu sana kama vile watu wanaofanya kazi za ofisini hufanya wanapoenda likizo. Asilimia 50 hivi ya aina hiyo ya kansa hutokana na mabaka meusi hasa kwenye sehemu ya juu ya mgongo na sehemu ya chini ya miguu.
Aina hii ya kansa ndiyo hatari zaidi kwa kuwa isipotibiwa mapema, inaweza kuvamia tabaka la ndani la ngozi, ambako kuna mishipa ya damu na limfu. Kuanzia hapo, inaweza kuenea haraka. Mtalaamu wa matibabu ya uvimbe Dakt. Larry Nathanson anasema: “Jambo la kushangaza ni kwamba kansa inayoathiri chembe za ndani za ngozi inaweza kutibiwa kwa urahisi inapogunduliwa mapema. Kwa upande mwingine, inapoenea haiwezi kutibiwa kwa dawa au mnururisho.” Kwa kweli, ni asilimia 2 au 3 tu ya wagonjwa wenye kansa hiyo iliyoenea ambao huweza kuishi kwa miaka mitano. (Ona dalili za mapema za kansa hiyo kwenye sanduku katika ukurasa wa 7.)
-
-
Linda Ngozi Yako!Amkeni!—2005 | Juni 8
-
-
Australia ina kiwango cha juu cha visa vya ugonjwa wa kansa ya ngozi, hasa ile inayoathiri chembe za ndani za ngozi.b Hii ni kwa sababu wakazi wengi wa nchi hiyo ambao walihama kutoka Ulaya Kaskazini wana ngozi yenye rangi hafifu, na wengi wao huishi pwani yenye fuo zenye jua. Uchunguzi waliofanyiwa wahamiaji hao unadokeza kwamba wale wanaohamia Australia wakiwa wachanga hukabili hatari kubwa zaidi ya kupatwa na kansa inayoathiri chembe za ngozi za ndani, jambo linaloonyesha umuhimu wa kujifunza tangu utotoni kuhusu madhara ya kupigwa na jua. Serikali ya Australia imeanzisha kampeni kali ya kuwafunza watu kuhusu hatari za jua kwa kuwaambia wavae t-shati, kofia, na kujipaka losheni ya kujikinga na jua. Mabadiliko hayo madogo katika mtindo wa maisha yamekuwa na matokeo makubwa katika kuzuia kansa inayoathiri chembe za ndani za ngozi kati ya vijana nchini humo.
-
-
Linda Ngozi Yako!Amkeni!—2005 | Juni 8
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 7]
DALILI KUU ZA KANSA HATARI
1. Mara nyingi uvimbe ambao haujakomaa wa kansa inayoathiri chembe za ndani za ngozi huwa na pande mbili ambazo hazitoshani. Mabaka ya kawaida huwa ya mviringo na pande zinazotoshana.
2. Mara nyingi uvimbe ambao haujakomaa wa kansa inayoathiri chembe za ndani za ngozi huwa na kingo zenye maumbo au mikato isiyotoshana. Mabaka ya kawaida huwa na kingo laini zilizotoshana.
3. Dalili za kwanza za kansa inayoathiri chembe za ndani za ngozi ni mabaka yenye rangi ya kahawia, hudhurungi, au nyeusi. Kansa hiyo inapoenea, huenda rangi hizo zikabadilika na kuwa nyekundu, nyeupe, na buluu. Mabaka ya kawaida huwa ya rangi ya kahawia.
4. Uvimbe ambao haujakomaa wa kansa inayoathiri chembe za ndani za ngozi huwa mkubwa zaidi kuliko mabaka ya kawaida nao huwa na kipenyo cha zaidi ya milimita sita.
[Hisani]
Chanzo: Taasisi ya Kansa ya Ngozi
Skin samples: Images courtesy of the Skin Cancer Foundation, New York, NY, www.skincancer.org
-