Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Uogope Kupigwa na Jua?
    Amkeni!—2009 | Juni
    • Kuharibika kwa Ngozi

      Kati ya visa vyote vya kansa ulimwenguni, asilimia 33 ni kansa ya ngozi. Kila mwaka, visa 130,000 hivi vya kansa inayoathiri chembe za ndani ya ngozi huripotiwa. Hiyo ndiyo kansa hatari zaidi ya ngozi. Kati ya visa milioni mbili na milioni tatu vya kansa nyingine za ngozi kama vile kansa inayoathiri chembe za katikati za ngozi na kansa inayoathiri chembe za juu za ngozi huripotiwa. Inakadiriwa kwamba watu 66,000 hivi hufa kila mwaka kutokana na kansa ya ngozi.a

      Miale ya jua inaweza kuharibu ngozi yako jinsi gani? Kuunguzwa na jua ndiyo madhara yanayojulikana zaidi ya kupigwa na jua kwa muda mrefu. Dalili zinazoonekana kwanza zinaweza kuendelea kwa siku kadhaa na zinaweza kutia ndani malengelenge na kubambuka ngozi.

      Ngozi inapounguzwa, miale hatari ya jua huua chembe nyingi zilizo katika tabaka la juu la ngozi na kuharibu matabaka ya ndani. Unaweza kujua ngozi ya mtu imeharibika rangi yake inapobadilika kwa sababu ya kupigwa na jua. Mtu anaweza kupatwa na kansa wakati chembe za DNA zinazodhibiti ukuzi na kugawanyika kwa chembe za ngozi zinapoharibiwa.

  • Je, Uogope Kupigwa na Jua?
    Amkeni!—2009 | Juni
    • Hivyo basi, miale ya jua inaposababisha kansa inaweza kuathiri sehemu mbili. Kwanza, inaweza kuharibu chembe za DNA, na pili, kupunguza uwezo wa asili wa kinga ya mwili wa kukabiliana na madhara hayo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki