-
Je, Kweli Ulimwengu Ulikuwa na Mwanzo?Amkeni!—1999 | Juni 22
-
-
Darubini kubwa sana yenye sentimeta 254 iliyowekwa kwenye Mlima Wilson kule California ilifanya iwezekane kupata uthibitisho huo. Mambo yaliyoonwa kupitia darubini hiyo katika miaka ya 1920 yalithibitisha kwamba ulimwengu unapanuka!
Awali, darubini kubwa zaidi zingeweza kutambulisha nyota moja-moja zilizokuwa katika kundi letu la nyota la Kilimia pekee. Ni kweli kwamba watazamaji wameona madoa ya nuru hafifu yanayoitwa nebula, lakini kwa ujumla madoa hayo yalidhaniwa kuwa mawingu ya gesi fulani katika kundi letu lenyewe la nyota. Lakini kwa kutumia darubini hiyo kali sana ya Mlima Wilson, Edwin Hubble alitambulisha nyota moja-moja katika nebula hizo. Madoa hayo ya nuru hafifu hatimaye yalitambulishwa kuwa makundi ya nyota kama tu Kilimia yetu.
-
-
Je, Kweli Ulimwengu Ulikuwa na Mwanzo?Amkeni!—1999 | Juni 22
-
-
Darubini ya Mlima Wilson ilisaidia kuonyesha kwamba ulimwengu wetu ulikuwa na mwanzo
-