-
Mungu Yumo Katika Hekalu Lake TakatifuUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Rekodi yataarifu: “Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu;
-
-
Mungu Yumo Katika Hekalu Lake TakatifuUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
12. Isaya aona madhabahu gani, na moto husababisha nini?
12 Mtajo “madhabahu” watukumbusha tena kwamba hilo ni ono. (Linganisha Ufunuo 8:3; 9:13.) Ndani ya hekalu huko Yerusalemu, mlikuwemo madhabahu mawili. Kabla tu ya pazia la Patakatifu Zaidi Sana palikuwa madhabahu ndogo ya uvumba, na mbele ya mwingilio kwenye patakatifu palikuwa madhabahu kubwa ya dhabihu, ambapo moto ulikuwa ukiwaka daima. (Mambo ya Walawi 6:12, 13; 16:12, 13) Lakini madhabahu hizo za duniani zilikuwa za mfano, ziliwakilisha mambo makubwa zaidi. (Waebrania 8:5; 9:23; 10:5-10) Mfalme Solomoni alipolizindua hekalu, moto kutoka mbinguni ndio ulioteketeza matoleo ya kuteketezwa juu ya madhabahu. (2 Mambo ya Nyakati 7:1-3) Sasa pia moto kutoka katika madhabahu ya kweli, ya mbinguni, ndio unaoondoa uchafu wa midomo ya Isaya.
-