Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuponda Kichwa cha Nyoka
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na wao wakaja kwenye uhai na wakatawala wakiwa wafalme pamoja na Kristo kwa miaka elfu moja.” (Ufunuo 20:4c, NW)

  • Kuponda Kichwa cha Nyoka
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 13. (a) Inatupasa tuoneje miaka elfu ambayo katika hiyo 144,000 hutawala, na kwa nini? (b) Papiasi wa Hierapolisi aliionaje miaka elfu? (Ona kielezi cha chini.)

      13 Kutawala na kuhukumu kwao kutakuwa kwa miaka elfu moja. Je! hii ni miaka elfu moja halisi, au inatupasa tuione kwa njia ya ufananisho kuwa ni kipindi kirefu cha wakati, kisichodhihirishwa? “Maelfu” yaweza kumaanisha hesabu kubwa isiyodhihirishwa, kama vile kwenye 1 Samweli 21:11. Lakini hapa “elfu” ni halisi, kwa kuwa inaonekana mara tatu katika Ufunuo 20:5-7 kama ile “miaka elfu.” Paulo aliita wakati huu wa hukumu “siku moja” alipotaarifu: “Yeye [Mungu] ameweka siku moja ambayo katika hiyo yeye anakusudia kuhukumu dunia inayokaliwa kwa uadilifu.” (Matendo 17:31, NW) Kwa kuwa Petro anatuambia kwamba siku moja kwa Yehova ni kama miaka elfu moja, inafaa kwamba hii Siku ya Hukumu iwe miaka elfu moja halisi.c—2 Petro 3:8, NW.

  • Kuponda Kichwa cha Nyoka
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Lakini wao watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, na watatawala wakiwa wafalme pamoja na yeye kwa miaka elfu.” (Ufunuo 20:6b, NW) Wakiwa pamoja na Yesu, watafanyiza serikali iliyo pekee kwa miaka elfu moja. Utumishi wao wa kikuhani, katika kutumia ubora wa dhabihu kamilifu ya kibinadamu ya Yesu, utainua binadamu watiifu wafikie ukamilifu wa kiroho, kiadili na kimwili. Utumishi wao wa kifalme utatokeza kujengwa kwa jamii ya kibinadamu ya tufe lote inayoonyesha uadilifu na utakatifu wa Yehova. Wakiwa mahakimu kwa miaka elfu moja, wao, pamoja na Yesu, wataongoza kwa upendo wanadamu waitikifu kuelekea mradi wa uhai wa milele.—Yohana 3:16.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki